Jengo la NSSF Hifadhi lililo karibu kabisa na mzunguko wa sanam ya Askari Posta halina huduma ya lift huu ni mwezi wa tano sasa. Jengo hili lina urefu wa ghorofa kumi na inawalazimu wapangaji kutumia ngazi kwa muda wote huo bila kujali ni mzee,mlemavu wala mgonjwa. Lifti imeshawekwa na wachina ila cha ajabu wameiwasha kama siku tatu halafu wakaizima...Kumbukeni mliahidi ni miezi mitatu tu ya kukosa huduma ya lift na sasa ni mwezi wa tano...Tunalipa kodi tunahitaji huduma yakuridhisha. ACHENI UBABAISHAJI.