Nsaku ne Vunda; Balozi wa kwanza kutoka Afrika

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
NSAKU NE VUNDA; BALOZI WA KWANZA KUTOKA AFRIKA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Friday-10/06/2022
Marangu, Kilimanjaro, Tanzania

Pichani ni Nsaku Ne Vunda, huyu bwana ndio balozi wa kwanza kutoka Afrika kwenda Ulaya, alikuwa mwanasiasa na mwanadiplomasia wa kwanza kutoka Afrika kuwakilisha Vatican na nchi kadha duniani.

Huyu alitoka Ufalme wa Kongo (jana niliweka makala yake hapa), huyu ndio mwanadiplomasia wa kwanza wa Kiafrika kwenda kuwakilisha nchi yake nje, alikuwa balozi wa Ufalme wa Kongo aliyeiwakilisha nchi yake katika nchi za Uhispania, Brazili, Ureno na Vatikani (Wakati wa utawala wa Papa).

Kwa heshima yake, ya kuwa mtu wa kwanza mweusi kuiwakilisha kanisa duniani alipo fariki alizikwa kwa amri ya Papa Paulo V katika Basilica ya Santa Maria Maggiore (moja ya Basilicas nne za Papa zinazoheshimiwa san), huko Roma, kwa heshima ya mazishi ya Kikristo.

Pia picha yake iliyochorwa imewekwa katika Jumba la Quirinale, (Ikulu ya zamani ya Papa na Ikulu Rasmi ya sasa ya rais wa Italia), huko Roma.

Nsaku Ne Vunda, pamoja na kuwa Mwafrika wa kwanza kuiwakilisha nchi yake (Kingdom of the Kongo) huko Roma, mwaka 1608, pia alikuwa balozi wa pili asiye toka Ulaya katika Holy see huko Vatican, wa kwanza alikuwa ni Mjapani Hasekura Tsenenaga, aliyewakilisha Japani huko Roma mnamo 1582.

Nsaku Ne Nvunda anachukuliwa kama ndio mwasisi na Baba wa diplomasia ya Angola na Afrika nzima na mtangulizi aliye anzisha uhusiano wa Italia na Angola.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 2256420

FB_IMG_1654864968871.jpg
 
Back
Top Bottom