Championship
JF-Expert Member
- Aug 7, 2019
- 5,499
- 10,540
Weka screenshot ya salio tuhakikishe. Nakuwekea screenshot yangu ya mwaka jana, sasa hivi nimeshaongeza sana mtaji. Na wewe weka yakwako tupate kuwa motivated.Hongera sana. Kadiri unavyo invest kwa muda mrefu zaidi, ndivyo return inavyokuwa kubwa. Mimi tangu nianze ajira yangu ya kwanza mwaka 2015, niliazimia monthly kuweka zaidi ya asilimia 70 ya mshahara wangu UTT kwa sababu sikuwa na sina muda wa kusimamia biashara actively. Nikatumikia committment yangu kwa uaminifu mkubwa.
Kuna miezi nilikuwa nje ya ajira lakini sikutoa hela yangu UTT. Mwishoni wa mwaka 2023, nilikuwa na milioni 200 kwenye account yangu ya Liquid fund.
January 2024 nikatoa milioni 70 nikanunua kiwanja cha square meter 1900 bunju B chenye foundation ya ujenzi tayari.
Malengo yangu ifikapo mwaka 2030 niwe na hela isiyopungua milioni 700 kwenye account yangu ya UTT liquid + hela yangu ya nssf nitakuwa na kama milioni 800 hivi.
Then nimepanga baada ya hapo kutoa milioni 200 nijenge kwenye hicho kiwanja na hela inayobaki nahamishia mfuko wa bond ili niweze kupata mshahara wangu wa kila mwezi from UTT bila jasho. I want to retire at age 42. Tuendelee kufukuzia malengo mkuu...
malembeka18 Englishlady macho_mdiliko hata sasa hivi utt inawekeza kwa kuikopesha serikali. Hakuna namna serikali inaweza kuchota fedha huko.
Kuogopa hapa ni sawa na kusema serikali inaweza kuja kwenye akaunti yako ya benki na kuchukua hela.
Msimamizi wa utt ni crdb bank na kila mwaka kuna mkutano na ripoti ya ukaguzi inatolewa.