Sababu haikuwa Mwanamke, ilikuwa ni STYLE ya uimbaji mashairi.
Kumbuka Tupac alianza kwa kutumia nyimbo za zamani za R&B na kuziwekea RAP. B.I.G. na yeye akaja na wimbo wa JUICY ambao ulitokana na wimbo wa Mtume (Juicy fruit - wimbo naupenda hadi leo) na akaja kuongeza wimbo wa Miss U\Mo money, Mo problem (Coming out) kutoka kwa Diana Ross.
Tupac alikuwa zaidi akim-copy Roger Troutman ambaye alikuja kumshirikisha moja kwa moja kwenye wimbo wa California Love. Nyimbo nyingi hasa kwenye Album ya Me against the World, utasikia style ya Roger.
Wimbo wa Me against the World ndiyo wimbo pekee ambao bila ya kufanyiwa PROMO (Tupac alienda jela), wimbo wenyewe ulijipaisha kwa watu kununua na kusikiliza sana na Mdj kuwa wanaupiga hadi ukashika namba moja.
kutoka wikipedia:
Me Against the World, released while Shakur was imprisoned, made an immediate impact on the charts, debuting at number one on the Billboard 200. This made Shakur the first artist to have an album debut at number one on Billboard 200 while serving time in prison.
Nafikiri tofauti kubwa ya BIG na Pac ni kuwa, PAC alikuwa ni zaidi ya Mwanamuziki. Alikuwa kama Activist fulani hivi na kiongozi mzuri sana. Ndiyo maana alivyoingia Death Row Records, aliwakusanya watu mashuhuri sana kwa muda mfupi na kuwaweka kufanya naye kazi. Alizungukwa na watu wakali sana kwenye mambo ya miziki na nafikiri alishakuwa tayari kuanza kufanya kazi na Legend Producer, Quncy Jones kama Baba Mkwe kwa mwanae Kidada Jones.
Kumbuka Album ya mwisho ya Pac, walishiriki watu kama George Clinton (Dog Original), Dr Dre, Snoop Dogg, Roger Troutman na wengine wengi ambao waliifanya album ya all eyes on me ipendwe hadi leo.
Hapo juu ni Tupac akiwa na Roger Troutman ambaye anaonekana anatesa na kinanda chake cha Talk Box, made by YAMAHA for Special Request.
na ugumu wao waligombana na kuuana kwa ajili ya mwanamke.
Chezea utamu wa kitumbua wewe?