Noti aina mbili kwenye mzunguko

rugo

Member
Jun 20, 2012
28
12
Kama sikosei karibu mwaka sasa Tanzania katika mzunguko kuna noti za aina mbili tofauti. Noti hizo ni Tshs. 500, 1,000, 2,000, 5,000 na 10,000 mpya na za zamani zote zinaendele kutumika, na hadi sasa sijasikia tamko la serikali kuhusu mwisho wa kutumika zile za zamani. Cha kushangaza zaidi ni kwamba, noti za zamani nazo bado zinaendele 'kufyatuliwa mpya'.

Kuna mambo mawili yananijia kichwani mwangu, inawezekana;
1. Huenda ndo mambo yetu yale ya 'Commission mlungula' au 'ten percent' (10%) na
2. Gavana wa sasa alitaka naye saini yake ionekane katika noti.

Bila shaka huu ndo udhaifu wa raisi wetu.

Nawasilisha.
 
Ni udhaifu wa hali ya juu maana inawachanganya kweli wageni na sisi tunachekelea kama majua
 
Wameshajua kuwa noti zao ni fake, ndo maana wanashindwa kutoa hizi za zamani.
 
Hali ya nchi yetu si nzuri kabisa...inafikia kipindi hatuwezi kufanya chochote! yani kila kitu hovyo tu!
Imefikia muda mtu unaangalia taarifa ya habari kuanzia stori ya kwanza mpaka habari za michezo zinaisha, hamna jipya kila unachoona na kusikia unasikitika!
 
dah nimekuelewa mkuu yaani kuanzia mwanzo wa taarifa ya habari ni drama tu hadi mwisho . hakuna habari ya kufurahisha wala kutia matumaini. ukija kwenye michezo ndio laana tupu watu wanaagwa wanaenda Olympic lakini kila mwananchi hata watoto wadogo wanajua matokeo. na yanakuwa hayohayo. lakini bado wanaenda tena na ahadi kibao. anyway tutafika
 
Mkuu katika hili nihofu hili lifuatalo ndilo linaloendelea.
Kwanza tumezoea toka enzi za mwalimu noti zikibadilishwa inatangazwa siku ya mwisho ya kubadili hela,kwa safari hii haikua hivyo,kwa sababu hiyo napata masha kuwa,huenda kuna vigogo wa serikali walishaiba/kuiba fedha nyingi serikalini,fedha ambazo walishindwa kuzipeleka akaunti za nchi za mbali kuzificha kwakua siku hizi huwaumbua,na walishindwa kuziweka kwenye akaunti zao kwa hofu ya kujulikana,wakaamua kuzichimbi ndani mwa majumba yao.Hivyo basi unapobadilisha noti na ukaweka siku ya mwisho inamaana unawafanya waanze kuzitoa ndani kwa mkupuo kitu ambacho kitakua kigumu kutekelezeka,na ndio maana wakamua kuziacha zote ziwe kwenye mzunguko ili wawe wanabadili taratibu,siku wakisha badili zote zikaisha mahala walipozificha ndipo watatangaza siku ya mwisho.Hii ndio serikali dhaifu
 
Kama sikosei karibu mwaka sasa Tanzania katika mzunguko kuna noti za aina mbili tofauti. Noti hizo ni Tshs. 500, 1,000, 2,000, 5,000 na 10,000 mpya na za zamani zote zinaendele kutumika, na hadi sasa sijasikia tamko la serikali kuhusu mwisho wa kutumika zile za zamani. Cha kushangaza zaidi ni kwamba, noti za zamani nazo bado zinaendele 'kufyatuliwa mpya'.

Kuna mambo mawili yananijia kichwani mwangu, inawezekana;
1. Huenda ndo mambo yetu yale ya 'Commission mlungula' au 'ten percent' (10%) na
2. Gavana wa sasa alitaka naye saini yake ionekane katika noti.

Bila shaka huu ndo udhaifu wa raisi wetu.

Nawasilisha.
:first:
 
Mtoa hoja unayo hoja. Lolote lawezekana kwenye nchi inayoendeshwa kwa auto pilot. Hebu fikiria ilipoibuka kashfa ya meli za mafuta za Iran kutumia bendera yetu. Hakuna aliyehangaika na kutoa maelezo wala wananchi hawakujisumbua kuisumbua hata kuiwajibisha serikali. Kila kitu cha hovyo kinawezekana Tanzania. Kwa ufupi ni kwamba genge dogo la wezi limeiuza na kuitumia Tanzania kama lipendalo kwa maslahi yake uchwara na hovyo.
 
Huwa nawashangaa wabunge wetu wakihoji vitu halafu vinaishia hewani hivi huwa ni nguvu ya soda au moto wa kifuu. maana mwisho wa siku bajeti inapita na wao wanakuwa kimya maadamu wameshajipatia posho yao ya siku. sioni wabunge wenye nafuu si wa magwanda, magamba au vikofia wote sawa boti iliyowabeba ni moja hayo mengine ni madoido tu.
 
Back
Top Bottom