Norway: Tumeguswa na kuzorota kwa haki za binadamu nchini Tanzania. Norway hutoa msaada mkubwa kwa Tanzania kuliko nchi yoyote Duniani

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Nchi ya Norway imesema imeguswa na kuzorota kwa haki za binadamu nchini Tanzania.

Kwa tusiofahamu, nchi ya Norway ndio hutoa msaada mkubwa wa kifedha kwa Tanzania kuliko nchi yoyote Duniani, sio hata wachina tunaosema ni rafiki zetu. Kwa miaka zaidi ya 60 Norway imekua ndiyo nchi inayoisaidia Tanzania kwa sehemu kubwa na wamekua partners wetu kwa miaka zaidi ya 60 kupitia Norad agency.

Kufahamu zaidi, nchi za Nordic kama Norway, Denmark, Finland ndizo nchi pekee ambazo zimekua na sisi katika hali zote kwa misaada. Miradi mingi ya umeme na maji nchi hii imefadhiliwa na Nordic countries bure kabisa.

Miaka ya 80 wakati Benki ya Dunia imemuwekea vikwazo Mwalimu Nyerere, nchi pekee ambazo zilikua zinatusaidia ni Nordic countries.

Sijui tumekosea wapi sasa kuwaudhi hata marafiki zetu wa kweli na sasa tunadhani wanafiki wachina ndio marafiki kisa tu walijenga TAZARA na kiwanda cha Urafiki ambacho kimekufa na kwakua hawatuulizi kuhusu haki za binadamu hata ukiua watu 800 hawakuulizi basi tunadhani ndio wazuri. Yaani watu ambao ukifanya uovu dhidi ya binadamu wenzako hawakuulizi na wanakupa hela ndio tunaona wazuri.

Sijui tunakosea wapi. Kwa kweli bado hatujakua na uwezo na nguvu ya kutunishiana misuli na hawa watu. Tuangalie yasije kutukuta ya Zimbabwe.

=====

POSTED BY: VICTORIA GARZA 10. AUGUST 2019

Norway is concerned about human rights in Tanzania

Norway is concerned about the human rights situation in Tanzania, which over the past 50 years has received more Norwegian assistance than any other country.

“We are concerned about the development of the human rights situation in Tanzania, including for the freedom of the press,” State Secretary Marianne Hagen (H) tells Bistandsaktuelt.
Tanzania became a main Norwegian partner country in the 1960s and has since received close to NOK 19 billion in aid from Norway, according to an overview from Norad.

In 2018, the assistance amounted to almost NOK 400 million, and more than 40 per cent of this went through the country’s authorities.

Last week, one of the country’s leading journalists, Erick Kabendera, was arrested, charged with organized crime, money laundering and tax evasion. He works for the British Guardian and Economist, among others.
Tanzania


“On Thursday, another critical research journalist was arrested, and the Norwegian Foreign Ministry is following this development with concern,” Hagen informs.

“Human rights are on the agenda in the regular political consultations between Norway and Tanzania, taken up in political meetings and followed up by the embassy in Dar es Salaam,” she continues.

“We will also scale up support for independent human rights organizations. This is important for promoting democracy and human rights,” Hagen concludes.

 
Mabeberu mnaruka na kukanyagana, hamna nafasi awamu hii...kama umetusaidia zaidi ya miaka 80 so what? Sisi tunaelekea uchumi wa kati soon tutajitegemea.
Kwani sasa tuko uchumi wa wapi mkuu?

Huo uchumi wa kati tunafika lini? Tunatokea upande gani kuelekea huko kati?

Eti so what? Ungekua umekufa kwakipindupindu bila misaada yao.
 
Du!. Naona baada ya kusakamwa na wale mabeberu wakuu wawili, UK na US, sasa wadau wengine wa maendeleo wanafuatia. Hii issue ya Kabendera isipokuwa handled with care and justly, sasa hivi inakwenda ku steal the limelight of SADC meeting.

Nchi inayoongoza kwa misaada kwa Tanzania ni Uingereza kipitia DFID, UKAID ambao hichangia 80% kwenye Busket Fund ya General Budget Support, halafu washirika wengine wa maendeleo ndio wanachangia ile 20%.

Norway ndie the biggest donor kati ya donors wote wa Nordic Countries.
P
 
Tunataka vitendo siyo blah blah, maneno wanayatoa kwa sababu mnawafwata na kuwabembeleza watoe tamko, lkn hiyo ni hewa tupu.

Siku nikiona Balozi wa USA katoka kuongea rasmi ndo nitaamini, kinyume na hapo ni matamko tu ya kulazimisha ambayo hata Mimi naweza kwenda Ubalozini kusema mtaani kwetu kuna gay ananyanyaswa tafadhali naomba muandike jambo, sekretari atachapa kuweka muhuli na kunipa hiyo karatasi, mimi nitaenda kusema USA imesema, ...
 
Back
Top Bottom