Norway Nchi Bora Kuishi duniani, Tanzania ya 164 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Norway Nchi Bora Kuishi duniani, Tanzania ya 164

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Oct 7, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Norway Nchi Bora Kuishi duniani, Tanzania ya 164
  [​IMG]
  Vivutio vya Norway Wednesday, October 07, 2009 4:40 AM
  Nchi ya Norway ndiyo nchi bora kuliko zote duniani kutokana na maisha bora huku Niger ndio nchi choka mbaya kuliko zote duniani wakati Tanzania inashika nafasi ya 164 kati ya nchi 182 duniani. Norway imeendelea kushika nafasi ya kwanza kama nchi yenye maisha bora kuliko nchi zote duniani na watu wengi wangependa kuishi nchini Norway kutokana na vivutio mbali mbali, ilisema taarifa ya shirika la maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP.

  Nchi ya Niger ambayo imeathirika zaidi na vita na balaa la ugonjwa wa ukimwi, ndiyo inayoshika mkia katika nchi zote duniani.

  Takwimu za matokeo haya zilichukuliwa mwaka 2007 kabla ya msukosuko wa mfumo wa fedha duniani kuanza.

  Katika tatu bora kuna Norway, Australia na Iceland ambazo zimetajwa kuwa na maisha bora zaidi kuliko nchi zingine. Uingereza inashika nafasi ya 21 duniani.

  Katika nchi tatu za mwisho kuna Niger inayoshika mkia ikifuatiwa na Afghanistan na Sierra Leone.

  Takwimu hizo zilifanyika kwa kuangalia kipato cha taifa cha mwananchi, kiwango cha elimu na matarajio ya urefu wa maisha (life expectancy).

  Kwa kuangalia kiwango cha kipato cha Mtanzania kwa mwaka, kiwango cha elimu yetu na matarajio ya umri wa kuishi wa Mtanzania, Tanzania inashika nafasi ya 164 duniani.

  Raia wa Niger anatarajiwa kuishi miaka 50 wakati raia wa Norway anatarajiwa kuishi miaka 30 zaidi yake.

  Katika kila dola moja ambayo mtu mmoja nchini Niger anajipatia kwenye kipato chake, angekuwa nchini Norway angejipatia dola 85.

  Wajapan ndio watu wanaoishi miaka mingi kuliko wote duniani, wanakadiriwa kuishi miaka 82.7 wakati waafghanistan ndio wanaoishi miaka michache kuliko watu duniani, hutarajiwa kuishi miaka 43.6 tu.

  Katika nchi 10 zinazoshika mkia, nchi nyingi zaidi ni za Afrika. Nchi 10 zinazoshika mkia ni Guinea Bissau-173, Burundi-174, Chad-175, Jamhuri ya Congo-176, Burkina Faso-175, Mali-178, Jamhuri ya Afrika ya Kati-179, Sierra Leone-180, Afghanistan-181, Niger-182.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3280494&&Cat=1
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mhhh!

  Ama kweli tuko kubaya sana!

  Lakini mind you, kuna watu hapahapa Bongo wanaishi maisha ya dunia ya Kwanza, iwould say wako katika list ya nchi za group la 1 just because they have deprived the wealth of most Tanzanians!
   
 3. m

  mimi-soso Senior Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  chanzo cha habari please
   
 4. p

  p53 JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Sijafika Norway lakini hizi habari nilishawahi kuzisikia.Norway inasemekana haijaathirka na hii economic crisis.Siku moja nilikuwa naangalia tv program moja ya Norway walikuwa wanaelezea huu mgogoro wa uchumi duniani.Pale Norway kuna watu wamepoteza kazi pia lakini kuna mama mmoja aliyepoteza kazi alikuwa anahojiwa akasema anachokosa kwa sasa katika maisha yake ni kusafiri wakati wa summer lakini mengine yote hayajaharibika.
  Mkuu Denmark ya ngapi kwenye hiyo list?Nilipita mwaka jana mambo yao safi si kitoto!
   
 5. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Hio taarifa ya HDI imekuwa ikitolewa miaka nenda rudi na hakuna chochote.

  Kila siku tunajidanyanya kwa mikakati kama MKUKUTA, Millenium Goals ya 2015 na kadhalika huku watu wakiganga njaa.

  Hio taarifa ni kama kofi la usoni ambalo Tanzania inapigwa kwa kuzingatia kwamba ni miaka 48! imepita tangu tupate uhuru na bado zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanaishi kwenye umaskini wa kutupwa.
   
Loading...