Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,921
- 15,613
North Korea 'inasemekana' imerusha leo hii kombora 'linalodhaniwa' ni la balistiki, ambalo limelipukia angani, muda mchache baada ya kurushwa. Hayo yamezungumzwa na South Korea.
Cheong Seong-chang, mtafiti mwandamizi ktk Taasisi ya Sejong ameiambia AFP kuwa dalili zaashiria kuwa jaribio la leo la North Korea lilihusisha kombora kuubwa zaidi la balistiki kuvuka mabara (ICBM) liitwalo Hwasong-17.
Mtafiti huyo akaendelea kusema kuwa jaribio hili lililofeli litachunguzwa na kufanyiwa utafiti zaidi na North Korea. Inaweza ikachukua karibia majaribio matatu kuhakikisha kombora hilo limefanikiwa kufikia malengo ya North Korea. Mtafiti huyo akasema anategemea North Korea kufanya jaribio moja au mawili kabla ya April 15.
Hata hivyo, historia yaonesha North Korea iliisharusha makombora matatu ya balistiki ya kuvuka mabara (ICBM). Kombora la mwisho lilikuwa ni Hwasong-15 lilirushwa November 2017. Kombora hilo lilionesha uwezo mkubwa zaidi na linaweza kufika Washington pamoja na ardhi yote ya Marekani.

Picha: Kombora la Hwasong-17 likiwa kwenye gari ya kulibebea lenye pea ya matairi 11 (matairi 22) lilipooneshwa kwa mara ya mwanzo kwenye paredi ya kijeshi mjini Pyongyang mnano October 10, 2020