NORTH KOREA:YALIYOJIRI GENEVA-SWITZERLAND:

Mwakamajoka

Senior Member
Nov 21, 2017
170
149
Mjumbe/Mwakilishi wa Taifa la Korea Kaskazini amewaeleza wajumbe kwenye mkutano uliojikita kwenye sakata la kupunguza matumizi/uendelezaji wa silaha hatari za Kivita(Disarmament). Mkutano huo umefanyika Geneva-Switzerland, mjumbe kutoka Korea Kaskazini ameionya Marekani kuhusu mikakati yake anayoifanya kwenye eneo la Peninsula ya Korea.

Han Tae Song, ambaye ni balozi wa Umoja Mataifa anayeiwakilisha Korea Kaskazini amesema majaribio ya nyuklia yaliyofanywa na Pyongyang mwaka jana yameifanya nchi ya Korea Kaskazini kuwa Taifa la kinyuklia kwa njia/utaratibu salama na uwazi.

Han Tae Song akaendelea kusema mbele ya mkutano huo kwamba Taifa la Korea Kaskazini hatimaye limefanikiwa kupata kinga/ngao ya vita yenye nguvu na yenye uhakika, ambapo hakuna jeshi wala kitu chochote kinachoweza rudisha nyuma.

"Najikubali kusema kwamba nguvu ya nyuklia ya Taifa la Korea Kaskazini inauwezo wa kukengeusha/kuvuruga na kudhibiti vitisho vya aina zote za Kinyuklia kutoka kwa Taifa la Marekani na pia tuna Ngao imara yakumdhibiti Marekani asianzishe vita dhidi ya Taifa la Korea Kaskazini ", Han Tae Song.

Han Tae Song akaendelea kusema Korea Kaskazini haitaamua kutumia silaha zake za nyuklia mpaka uhuru wao na maslahi yao yatakapokiukwa/vurugwa na majeshi/mataifa yenye chuki dhidi yao.

Mjumbe (Han Tae Song) amehimiza kusitisha mazoezi ya vita ya nyuklia yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini kwenye eneo la Peninsula ya Korea, na amepinga uwepo wa mjeshi ya Marekani kwa Usalama wa wa Mashindano ya Olympic yatakayofanyika msimu wa baridi kuanzia 9/2/2018.

Mjumbe kutoka Marekani kwenye mkutano huo ameunga mkono mpango wa Korea Kaskazini kusitisha mipango yake ya Nyuklia na kuongezewa vikwazo dhidi ya Taifa la Korea Kaskazini. Akamaliza kwa kusema Marekani haitakubali Korea Kaskazini kuwa Taifa la Nyuklia.

RT,
Published: 23 Jan 2018/12:23 GMT
 
wameshiba hao... hacha sisi wenye njaa endelee kupiga miyayo... huku tuki kiangalia chakula
 
North Korea anasema tayari ni nyuklia state marekani anasema hatokubali korea kaskazini iwe na uwezo wa nyuklia hapo nashindwa kuelewa!!
 
NK Imeshakuwa nuclear state.

Halafu ni jambo gumu kuwazuia wanachokiamini dhidi ya Marekani.
 
North Korea anasema tayari ni nyuklia state marekani anasema hatokubali korea kaskazini iwe na uwezo wa nyuklia hapo nashindwa kuelewa!!
Marekani kwa usalama wake na washirika wake hakubali Korea Kaskazini awe Nuclear State, kwa maana ya kwamba Korea Kaskazini aachane na mipango ya Silaha za Nyuklia(Nuclear warheads) na viwango vyote kwa makombora ya masafa marefu.

1: Short range Ballistic Missile
2: Intermediate Ballistic Missile
3: Intercontinental Ballistic Missile


Marekani anafahamu kwamba Pyongyang wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa ubunifu na ubora wa makombora yote yanayomilikiwa na taifa la Korea Kaskazini.

Kwa mtazamo wangu, kuna nchi zinazo amua nani awe Nuclear State na nani asiwe Nuclear State, mmoja wao ni Marekani. Marekani hajakubali Korea Kaskazini aingie kwenye Nukes Club States. Ukizingatia umiliki wa Silaha za Nyuklia na Makombora ya masafa marefu Korea Kaskazini ni Nuclear State ila hajaidhinishwa kuwa Nuclear State na kuingia kwenye Nukes Club.
 
North Korea anasema tayari ni nyuklia state marekani anasema hatokubali korea kaskazini iwe na uwezo wa nyuklia hapo nashindwa kuelewa!!
N.Korea bado hawajawa nuclear state bado wanajaribujaribu!
 
Back
Top Bottom