North Korea says; It will be An All Out War

chifu77

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
902
595
Heshima kwenu wakuu.
Fita ni fita mura.. makamu wa rais wa marekani yuko ziarani katika nchi 4 zikiwepo south korea, japan, indonesia.. wachambuzi wanasema ziara yake inalenga kuweka mambo sawa kwa washirika muhimu hasa kupata maeneo ya ardhi, anga na bahari watakayotumia kumchakaza mkorea. Mike Pence alikaririwa akisema " the era of strategic passion was over" kwamba zama za obama za kuishi kwa makubaliano na ahadi zimekwisha.

Naye mzee trump amesema "mipango yote tayari ipo mezani"

Nao North korea wameweka wazi kuwa wataendelea kufanya majaribio ya silaha na makombora yao 'on weekly, monthly & yearly basis'. Wameonya kwamba endapo U.S.A watadhubutu kutumia jeshi dhidi yao.. basi watajibu mapigo kwa nguvu zote. "We will counter react with all our weapons & missiles using our own style and method; from day one onwards"

North korea wameonya kwamba kamwe hakuna mtu wa kuwaamulia maisha yao. Kwani wanajiamini katika waliyo amua kuyatenda.

Mpaka sasa hakuna nchi yoyote iliyokwisha tangaza kwamba wataunga mkono, upande upi. Ila inasadikika kuwa katika hii vita, marekani ina washirika wengi nyuma yake.

Joto la mapambano linazidi kupanda.
 
kama vipi waende mwezini wakapambane hayo manyuklia yao yatatuharibia dunia
 
Mbona jana huyo huyo Mike Pence akamalizia kwa kusema meza ya makubaliano bado ipo wazi, na Waziri wa Mambo ya Nje wa China akasema watasapoti chochote mradi kiwe ni mazungumzo yawe rasmi au siyo rasmi.

Sioni kama usa wana hamu na vita kwa aliyoyasema jana.
 
Mipango yote imekamilika kwa zaidi ya 100%; kinachosubiriwa ni signature ya Trump tu wanaume wamchakaze kiduku live. Signature ya Mzee Trump ndicho kitu pekee kilichoiweka dunia kwenye tension ya ajabu kuliko kitu kingine chochote kwa sasa. Hadi Makamu wa Rais wa US kutembelea DMZ na kuongea aliyoyaongea lile ni tangazo la vita kwa zaidi ya 50%. In short, kwa sasa vita haiepukiki tena. Kinachotakiwa ni kuomba isilete madhara makubwa.
 
Mbona jana huyo huyo Mike Pence akamalizia kwa kusema meza ya makubaliano bado ipo wazi, na Waziri wa Mambo ya Nje wa China akasema watasapoti chochote mradi kiwe ni mazungumzo yawe rasmi au siyo rasmi.

Sioni kama usa wana hamu na vita kwa aliyoyasema jana.
Jamaa wanajifanya kukubaliana na mazungumzo ila hawana imani na north korea. wanadai imepita miongo 2 tangu mwaka 1992 wanazungunza ila north korea wanageuka geuka.

So, wanasema dawa ni kuilipua hiyo mitambo ya nuklia na kumchakaza serikali yao
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mbona jana huyo huyo Mike Pence akamalizia kwa kusema meza ya makubaliano bado ipo wazi, na Waziri wa Mambo ya Nje wa China akasema watasapoti chochote mradi kiwe ni mazungumzo yawe rasmi au siyo rasmi.

Sioni kama usa wana hamu na vita kwa aliyoyasema jana.
Tangu China aseme hapo hakuna mshindi, marekani kaingia baridi! Anajitahidi kuchimba mkwara lakini wenye akili zao washajua kitumbua kimeingia Mchanga!
 
Korea ategemee Pre Emptive strikes kwenye ballacks zake, palace zake, radar zake, bases zake, camps zake
Hadi hapo atakuwa kesha punguzwa nguvu kwa 75pc kitakachofuata baada ya hapo ni wale wapinzani wa Kim kuanza chukua nchi taratiiiibu na kujiweka pale juu afu wao wataitupilia mbali China na kuwa wapenzi wa Skorea
 
Heshima kwenu wakuu.
Fita ni fita mura.. makamu wa rais wa marekani yuko ziarani katika nchi 4 zikiwepo south korea, japan, indonesia.. wachambuzi wanasema ziara yake inalenga kuweka mambo sawa kwa washirika muhimu hasa kupata maeneo ya ardhi, anga na bahari watakayotumia kumchakaza mkorea. Mike Pence alikaririwa akisema " the era of strategic passion was over" kwamba zama za obama za kuishi kwa makubaliano na ahadi zimekwisha.

Naye mzee trump amesema "mipango yote tayari ipo mezani"

Nao North korea wameweka wazi kuwa wataendelea kufanya majaribio ya silaha na makombora yao 'on weekly, monthly & yearly basis'. Wameonya kwamba endapo U.S.A watadhubutu kutumia jeshi dhidi yao.. basi watajibu mapigo kwa nguvu zote. "We will counter react with all our weapons & missiles using our own style and method; from day one onwards"

North korea wameonya kwamba kamwe hakuna mtu wa kuwaamulia maisha yao. Kwani wanajiamini katika waliyo amua kuyatenda.

Mpaka sasa hakuna nchi yoyote iliyokwisha tangaza kwamba wataunga mkono, upande upi. Ila inasadikika kuwa katika hii vita, marekani ina washirika wengi nyuma yake.

Joto la mapambano linazidi kupanda.

Kim safi sana babaa nakuminii.piga mbwa huyo mpaka atambue kuwa wewe mapanki ni nani
 
Hii inaitwa, kma mbwai mbwai

“Tutatekeleza majaribio zaidi katika kipindi cha kila juma,kila mwezi na kila mwaka,” alieleza makamu waziri wa masuala ya kigeni Han Song-ryol alipokuwa akizungumza na mwanahabari wa BBC, John Sudworth.
Awali, Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence aliionya Korea kutoijaribu Marekani, akisema kuwa muda wa kuivumilia nchi hiyo kwa miaka mingi umekwisha.
Bwana Pence aliwasili mjini Seoul nchini Korea Kusini mwishoni mwa juma lililopita baada ya Kombora la Korea kaskazini kushindwa kupaa.
Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika eneo la Peninsula, wakati huu kukiwa na hali ya kushambuliana kwa maneno baina ya Korea kaskazini na Marekani.
Bwana Han ameiambia BBC: “Ikiwa Marekani inapanga kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi yetu tutachukua hatua ya kupambana kwa shambulio la Nuklia kwa mbinu zetu na mtindo wetu.
 
Hii inaitwa, kma mbwai mbwai
Heshima kwenu wakuu.
Fita ni fita mura.. makamu wa rais wa marekani yuko ziarani katika nchi 4 zikiwepo south korea, japan, indonesia.. wachambuzi wanasema ziara yake inalenga kuweka mambo sawa kwa washirika muhimu hasa kupata maeneo ya ardhi, anga na bahari watakayotumia kumchakaza mkorea. Mike Pence alikaririwa akisema " the era of strategic passion was over" kwamba zama za obama za kuishi kwa makubaliano na ahadi zimekwisha.

Naye mzee trump amesema "mipango yote tayari ipo mezani"

Nao North korea wameweka wazi kuwa wataendelea kufanya majaribio ya silaha na makombora yao 'on weekly, monthly & yearly basis'. Wameonya kwamba endapo U.S.A watadhubutu kutumia jeshi dhidi yao.. basi watajibu mapigo kwa nguvu zote. "We will counter react with all our weapons & missiles using our own style and method; from day one onwards"

North korea wameonya kwamba kamwe hakuna mtu wa kuwaamulia maisha yao. Kwani wanajiamini katika waliyo amua kuyatenda.

Mpaka sasa hakuna nchi yoyote iliyokwisha tangaza kwamba wataunga mkono, upande upi. Ila inasadikika kuwa katika hii vita, marekani ina washirika wengi nyuma yake.

Joto la mapambano linazidi kupanda.

Hiroshima mpaka leo bado wanashuhudia madhara ya Bomu La Nyukria lililopigwa kwao. Sio jambo la kufurahia hili, hata robo.
 
Back
Top Bottom