Wanajukwaa, salaam!!!
Ni mwezi mmoja sasa tangu ninunue simu aina ya NOKIA E5-00 (brand new). Kwa bahati mbaya, kitabu cha maelekezo nilikipoteza.
Tangu kununua simu hii nimekuwa nikijaribu kuitumia kwa huduma ya internet (browsing), lakini imekuwa ikigoma, though nimejiunga/nimeisajili ili niweze ku-access internet.
Lakini kila ninapoanza ku-surf, baada ya kuweka website ninayoitaka, let say www.jamiiforums.com, imekuwa ikiniletea ujumbe unsupported scripts in contents na ninapo-click ok unatokea ujumbe unaosema insufficient memory. Meseji hizo zimekuwa zikitokea hata ninapokuwa ninapokea picha au nyimbo kwa njia ya bluetooth.
possible umejaza phone memory. Nokia nyingi ukijaza phone memory na ram inapungua so nakushauri nenda file manager then move picha videos na music kwenye memory card then jaribu tena.
kufanya firmware update ni lazima uwe na internet iliyo na kasi nzuri na ya uhakika na hakikisha pc yako iko na backup ya kutosha ktk power ili ikitokea umeme umekatika unaweza pc imalize zoezi ambalo hutumia takribani robo saa. Cha kufanya hakikisha una usb data cable ya simu yako alafu download nokia pc suite na uinstall kwa pc yako. Hapo ktk hiyo software kuna option hiyo ya kufanya update