NOKIA 2.1 ujio mpya

Kwa hiyo bei na specification ulizoweka nakushauri uangalie upande wa xiaomi.
 
Sure
 
Nokia iko vizuri sana.Ninatumia nokia 5.ina 13 primary camera na 8 front.ina Snapdragon na betri 3000amh.ina 16 gb internal memory.ina android 8.1,bei ni 450000tsh,Jumia.kila mwezi unapokea security patch level.Muda wowote itapata android pie,yaani android 9.Kwa kifupi Nokia wapo vizuri saaana,yaani full raha.Tayari Nokia kama 7.1,8, zimeshapata android pie.Karibu kwenye ulimwengu wa Nokia,ufurahie simu yako.Achana na viruses,achana na mauza uza ya simu kama tecno full wadudu.Tecno h6 ilinifanya niape kutumia tena tecno.
 
Kwa sisi watumiaji wa Nokia tayari December android security patch level kama huja update simu yako, waweza update kwani tayari ipo hewani.
 
usisahau na pacha wake nokia 8.1 iliyoachiwa juzi juzi.Namaanisha yule mtangulizi wa 8.1 yaani Nokia 8.Full mkwaju.
 
xiaomi au meizu ndo budget phones.... Hizi nokia ghali sana
Hapana mkuu,watu tu wamekariri.Nokia 1 kwa mfano jumia inauzwa 150000, Nokia 2 bei yake ni range ya 250000 to 300000.Angalia jumia kila kitu kiko wazi.Cha ajabu kuna watu wana nunua Tecno kwa range ya 250000-500000.
.Shida tunajitakia wenyewe
 
Sio kwa nokia mkuu
 
Mkuu RAM 1Gb ROM 8Gb!!!??? Mwaka 2018 SIKUSHAURI KABISA.

Dunia inapoelekea mkuu tafuta simu yenye Ram kuanzia 3Gb na Rom 32 Gb.
 
ukifananisha na tecno, tecno ni ghali lakini ukifananisha na hawa wachina wengine hata nokia ni ghali
 
ukifananisha na tecno, tecno ni ghali lakini ukifananisha na hawa wachina wengine hata nokia ni ghali
Tatizo ni kwamba unanunua kitu kwa bei kubwa wakati hakina ubora.Hapo ndipo tunapojitakia wenyewe haya majanga
 
Sure mkuj Nokia wamenivutia sana
 
Hizi Nokia mpya zote zinatumia Android one/Go hivyo zinapata updates punde Google wanapozitoa.

Hio 2 yako tayari ina android 8.1 na soon itapata android 9.
 
Mkuu mbona ya zamani hiyo, Mimi nina Nokia 5.1 ila sasa kuna toleo jipya 8.1 plus
Mkuu ka Samsung kangu kamechoka mbaya sasa simu ninayofikiria kuchukua kwa sasa ni Nokia baada ya hii Samsung... Sasa naomba unipe ubora wa Nokia 5.1(x5) maana nataka kununua Nokia kati ya hiyo x5 au x6, kama bajet ikitiki basi nitachukua 8.1 (x7)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…