GE2025 "NO REFORM NO ELECTION"Mkakati uliokosea Timing

GE2025 "NO REFORM NO ELECTION"Mkakati uliokosea Timing

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,127
Reaction score
1,634
Huwezi kupambana na kuleta mabadiliko makubwa ya kikatiba kwa Nchi ambayo imeongozwa na chama kimoja kwa zaidi ya miongo mitano kwa harakati za barabarani (maandamano & mikutano ya hadhara) na vikao vya majadiliano tu bila nguvu ya bunge, ni ngumu sana. Ili kulainisha mabadiliko haya lazima uwe na wabunge makini katika Bunge hata kwa uchache.

CHADEMA mwaka huu 2025 ilipaswa iingie kwenye uchaguzi kwa namna yoyote ile ili ipambane kupata Rais, Wabunge na Madiwani kwa katiba hii hii iliyopo. Who knows matokeo yangekuwaje? Lakini wasingekosa washindi kwa nafasi hizo. Who knows!!?

Tujiulize CHADEMA hii hii ilipomsimamisha Lowasa kugombea Urais si ilipata viti vingi tu vya wabunge kwa katiba hii hii!!!?

Tujiulize angelisimama Tundu Antipas Lisu ingekuwaje? Hata kama isingeshinda U Rais lakini wangepata viti vingi vya wabunge na Madiwani.

Kupitia hawa wabunge na harakati za barabani na vikao vya majadiliano kuelekea uchaguzi wa 2030 ndo CHADEMA ingelianza na utekelezaji wa mkakati wao wa NO REFORM NO ELECTION.

Basi itoshe kusema kama CHADEMA haitoshiriki katika uchaguzi wa 2025 itakuwa pigo la mageuzi ya kisiasa, ki Katiba, kiutawala na kiuchumi Nchini.

Muda bado upo. Ifanyike kila namna maridhiano yafanyike (vikao vya majadiliano) ili vyama vyote ikiwemo CHADEMA vishiriki uchaguzi hata ikibidi Uchaguzi usogezwe mbele na hii italeta hali ya maridhiano na kuboresha haki na usawa wa kisiasa Nchini.
 
Hakuna kuitwa ikulu kunywa kahawa,korosho na sharubati tena.
Jk aliwaita
SSH Aliwaita na alikuja na 4Rs bado mkanyea kambi
 
tatizo lissu anaona aibu kukubali ,,,hahahaha na nimwambie tu huko aliko kwamba , niemuandalia uzi matata wa kumnanga ! akilegeza tu ninae. hahahahahaha
 
"Ni maoni yako..."
CHADEMA ni chama kilichochezewa rough nyingi mno na wana-CCM.

'Ivo kwa uhamuzi waliouchukua ni sahihi pia, time will tell..

No reform, No election
 
1754572147122.jpg
 
Baada ya kushiba mnaropoka. Nyie endeleeni na uchaguzi iacheni CHADEMA na msimamo wake.
 
tatizo lissu anaona aibu kukubali ,,,hahahaha na nimwambie tu huko aliko kwamba , niemuandalia uzi matata wa kumnanga ! akilegeza tu ninae. hahahahahaha

Hata Ndugai alikuwa na kisirani kuliko wewe yeye ndio alimfukuza Lissu kwenye ubunge na kabla ya hapo alisitisha mshahara wake, ila Lissu bado yupo. Sembuse wewe kula kulala?
 
Biggest political miscalculation- blunder in history
 
"Ni maoni yako..."
CHADEMA ni chama kilichochezewa rough nyingi mno na wana-CCM.

'Ivo kwa uhamuzi waliouchukua ni sahihi pia, time will tell..

No reform, No election
Nadhani approach nzuri na ambayo ingeleta tija , ni kwanza kufanya Reform za ndani ya Chama chenu then ndo muangalie kutafuta reforms za nje. That would work well to achieve the Goal.
 
Misimamo isiyo na Faida kwa Chama wala kwa Taifa. Hiyo misimamo hasi ndo imeua Chama, hamuwezi kuwa mnakwenda tu kama Nyumbu bila hata kupata nafasi ya kusimama na kutafakari kama safari yenu hiyo mnayoenda iko kwenye njia sahihi ya kuweza kuwafikisha . Suala siyo kuanza safari , ni Kumaliza na kufika kule unako taka kufika, na hapo lazima uwe flexible kubadiri njia na hata kama ni kubadiri gear angani, kama ikibidi.
 
Hiyo keki inaenda kuchacha mikononi mwa wabebaji (waandamanaji, wapenzi, viongozi na wanachama wa CHADEMA) kwasababu walaji (Wabunge wa CHADEMA) hawajafika meza kuu (Bungeni). Uchaguzi huu wa 2025 CHADEMA ilipaswa iingie kama Kifaru aliyejeruhiwa. Chaka kwa Chaka. Najua vikwazo vingekuwa vingi lakini wangeliokota kitu.
 
Misimamo isiyo na Faida kwa Chama wala kwa Taifa. Hiyo misimamo hasi ndo imeua Chama, hamuwezi kuwa mnakwenda tu kama Nyumbu bila hata kupata nafasi ya kusimama na kutafakari kama safari yenu hiyo mnayoenda iko kwenye njia sahihi ya kuweza kuwafikisha . Suala siyo kuanza safari , ni Kumaliza na kufika kule unako taka kufika, na hapo lazima uwe flexible kubadiri njia na hata kama ni kubadiri gear angani, kama ikibidi.
Nilishangaa sana baada ya Uchaguzi wao wakaja na utekelezaji wa No reform no election. Ilipaswa wajidhatiti kwanza kwa kuimarisha nguvu yao ndani na nje ya Bunge kwa kushiriki uchaguzi then baada ya hapo ndo waje na utekelezaji wa agenda yao.
 
Huwezi kupambana na kuleta mabadiliko makubwa ya kikatiba kwa Nchi ambayo imeongozwa na chama kimoja kwa zaidi ya miongo mitano kwa harakati za barabarani (maandamano & mikutano ya hadhara) na vikao vya majadiliano tu bila nguvu ya bunge, ni ngumu sana. Ili kulainisha mabadiliko haya lazima uwe na wabunge makini katika Bunge hata kwa uchache. CHADEMA mwaka huu 2025 ilipaswa iingie kwenye uchaguzi kwa namna yoyote ile ili ipambane kupata Rais, Wabunge na Madiwani kwa katiba hii hii iliyopo. Who knows matokeo yangekuwaje? Lakini wasingekosa washindi kwa nafasi hizo. Who knows!!? Tujiulize CHADEMA hii hii ilipomsimamisha Lowasa kugombea Urais si ilipata viti vingi tu vya wabunge kwa katiba hii hii!!!? Tujiulize angelisimama Tundu Antipas Lisu ingekuwaje? Hata kama isingeshinda U Rais lakini wangepata viti vingi vya wabunge na Madiwani. Kupitia hawa wabunge na harakati za barabani na vikao vya majadiliano kuelekea uchaguzi wa 2030 ndo CHADEMA ingelianza na utekelezaji wa mkakati wao wa NO REFORM NO ELECTION.
Basi itoshe kusema kama CHADEMA haitoshiriki katika uchaguzi wa 2025 itakuwa pigo la mageuzi ya kisiasa, ki Katiba, kiutawala na kiuchumi Nchini.
Muda bado upo. Ifanyike kila namna maridhiano yafanyike (vikao vya majadiliano) ili vyama vyote ikiwemo CHADEMA vishiriki uchaguzi hata ikibidi Uchaguzi usogezwe mbele na hii italeta hali ya maridhiano na kuboresha haki na usawa wa kisiasa Nchini.

Kwanza jifunze kuandika vizuri

Weka space weka paragraph

Unaandika kama sisimizi wamebebana ?

Unaongea mambo makubwa ndio maana hata uwezi kuandika

Rudi darasani kajifunze kuandika vizuri
 
Honestly they have tried that lakini haikufanya kazi 2015 - 2020 mwisho viongozi waliochaguliwa kuenguliwa pasi utaratibu na kupata madhara. Ila swala je chadema kutoshiriki uchaguzi huu anapoteza nini hasa tofauti na nafasi?
 
Back
Top Bottom