Mbekengason
Senior Member
- Sep 27, 2013
- 187
- 41
Ni imani ya wananchi kuwa katika mfumo tulionao, chama kinachopata kura nyingi ktk uchaguzi mkuu kinaunda serikali. Kuanzia kwa rais hadi mtendaji wa kijiji. Hivo hamna chama wala serikali kwa mategemeo ya mwananchi. Kwa karibuni kumejitokeza mtiririko wa watendaji wakuu wa chama tawala kwenda kwa wananchi na kukuta hakuna chochote kilichofanyika katika kuwapatia maisha bora kama walivyohaidi na wanavyokuwa wanajinadi kuwa wamefanya.
Majigambo yao wanapotembea na kuambiwa na walio wao kuwa kilichokuwa kizuri hasa ktk miongo takrabani miwili kinapungua na kupungua. Maisha bora yanakuwa ya kufikirika. Wanaimbiwa tenzi za barabara za lami, shule za kata na pilau ktk mikutano. Wakisha shiba wanaanza kusema kuwa chakula kizuri kama hicho ni mara moja kwa mwaka, nyumba zetu ni mbavu za mbwa, nguo hata mtumba shida kununua maana bei ya mazao ni chini ya gharama ya uzalishaji, rushwa, ubadhirifu, uonezi na uzembe wa wateule wa chama tawala vimetamalaki.
Hapo huyo rangi ya njano utamsikia kuwa sio chama ni serikali.