Rutakyamilwa
JF-Expert Member
- Feb 27, 2009
- 1,872
- 1,235
Wanajamii, soma habari hii chini. Nimeichukua toka TIJA. WATANZANIA TULISHINDWA NINI KUENDESHA HII BANK, MAKABURU WANAWEZAJE[/I][/B]
QUOTED:
"Nakumbuka miaka michache iliyopita hii bank ikiwa mikononi mwa serikali ilikuwa inaendeshwa kwa hasara mpaka ikauzwa kwa makaburu."
NMB yapata faida ya bilioni 54
Benki ya NMB imepata faida ya shilingi bilioni 54 katika mwaka uliopita baada ya makato ya kodi, ambayo ni ongezeko la asilimia 13.56 kulinganisha na mwaka 2009.
NMB, ambayo ina jumla ya wateja milioni 1.4 hapa nchini, ilipata faida kabla ya makato ya kodi inayofikia shilingi bilioni 78 kwa mwaka 2010.
Hilo ni ongezeko kubwa kulinganisha na mwaka 2009 ambapo benki hiyo ilipata faida kabla ya makato ya kodi ya shilingi bilioni 68 na faida baada ya mapato ya kodi ya shilingi bilioni 47.55.
"NMB imepata mafanikio makubwa kwenye shughuli zake za kibenki na imeendelea kufanya vyema kutokana na mazingira mazuri ya uchumi yaliyopo hapa nchini," Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Mark Wiessing.
Wiessing alisema mahesabu ya mwaka 2010 ya NMB yameonesha kuwa benki hiyo imepata mafanikio makubwa kwenye shughuli zake kuu za kibenki, ikiwemo kufungua matawi mapya na kupata ongezeko la mapato yanayotokana na riba na mengineyo.
"Pamoja na kupunguza riba kwenye soko, faida ya benki kabla ya makato ya kodi iliongezeka mpaka kufikia shilingi bilioni 78 kutokana na mikopo, amana za wateja na ukuaji wa shughuli za kibenki kwa ujumla," alisema.
Alisema mapato ya jumla ya NMB yaliongezeka kwa asilimia 23 mwaka jana kutokana na kuongezeka kwa mapato yanayotokana na yasiyotokana na riba.
"Amana za wateja wetu zimekuwa zikionesha ukuaji mwaka hadi mwaka na kuongezeka kwa asilimia 24 mwaka jana hadi kufikia shilingi trilioni 1.8," alisema.
Alisema jumla ya rasilimali za benki hiyo (total assets) ziliongezeka kwa asilimia 26 mwaka jana hadi kufikia shilingi trilioni 2.1.
"Idadi ya wateja wa benki imeongezeka kufikia jumla ya wateja milioni 1.4 nchi nzima na zaidi ya wateja 400,000 wanatumia huduma za benki zinazotembea (mobile banking channel)," alisema.
Alisema kuwa NMB inatarajia kupata mafanikio makubwa zaidi kwenye kazi zake za kibenki kwa mwaka 2011 kutokana na kuendelea kuboresha huduma zake kwa wateja na kuimarika kwa uchumi wa nchi.
"NMB itaendelea na jitihada zake za kuboresha huduma kwa wateja kwenye kazi zake zote huku ikifanya shughuli zake za kibenki kwa umakini mkubwa," alisema.
CHANZO: NIPASHE
0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni