NMB yapandisha riba zao

Ok9

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
4,525
4,090
Riba za mikopo kwa NMB ilikuwa ni 18% lkn sasa ni 20%.
Kwa hali hii mbona maisha yanaenda kuwa magumu tena...
 
Nao wanaminywa na mifumo mibovu ya makato kutoka serikalini.....plus economic situation ya wananchi sasa.....hali imekuwa ni tete........hakuna pa kupumulia......pesa ambazo zilitakiwa ziwe kwenye uzalishaji zipo mikononi mwa walafiwachache na uzalishaji wa bidhaa na huduma halali kisheria vimeshuka......wadhani tutafika kwa style hiyo........so hiyo hali ya kupandisha riba si mwanzo ila ni matokeo tu ya mfumo m'bovu wa uongozi wa serikali iliyopo kwenye uongozi hivi sasa........!
 
Kukopa napo ni shidaaa, na biashara kupanuka bila mkopo ni shida zaidi
 
Kama nmb tulokuwa tunawaamini na 18%.....imefika hapo.... Je hawa wakopeshaj binafs kama Bayport itakuwaje
 
Kiutaratibu wanapaswa kutoa maelezo, kwanini wamepandisha riba ? , kinachotakiwa mikopo imnufaishe mtu has a wenye maisha maguhmu
 
Riba za mikopo kwa NMB ilikuwa ni 18% lkn sasa ni 20%.
Kwa hali hii mbona maisha yanaenda kuwa magumu tena...
Katika kanuni za uchumi, riba huwa inakuwa determined na mambo mengi kama vile risk, operation costs, na inflation. Hivyo ikiwa country's inflation rate is high then riba za mabank nazo zitakuwa kubwa...so jaribu kuangalia inflation rate yetu ndio utajua implication ya nmb kupandisha riba
 
Ni aibu sana nchi hii. Daah wafanyakazi jumapili tujitokeze tufanye yetu
 
Inakoelekea inflation itakua juu soon... maana mabenki yanaweza pata hasara sana sasa yanajihami
 
Dawa ni moja tu iondoe CCM madarakani. Kama kuna ndugu yako ana kiherehere cha kuipigia CCM kura, ficha kadi yake mapema, utampatia tarehe 25 saa 12 jioni.
 
Kwa Tanzania sioni ajabu kuona RIBA za mabenki zikiongezeka. Pamoja na sababu za kitaalamu lililo kubwa ni uongozi mbovu na dhaifu. Hili ndilo kubwa.

Kwa sababu za kitaalamu RIBA huongezeka pale mfumuko wa bei unapokuwa juu. Kwa nchi yetu mfumuko ukiwa tarakimu moja (single digit) hali sio mbaya lakini ukiwa zaidi ya tarakimu moja (Mfano 10,11,12.....) hali sio nzuri. Tujiulize je, mfumuko umeongezeka?
Sababu nyingine ni serikali kukopa kwenye mabenki. Hali hii huchangia riba kupanda.
Riski za ukopeshaji zinapoongezeka huchangia kuongeza riba.
Wateja kutokuwa na weledi na mwamko wa kudai haki Zao. Kwa nchi za wenzetu Kuna Chama cha wakopaji na wenye kutumia huduma za kifedha. Riba haiwezi kupanda pasipo chama hiki kukaa mezani na taasisi husika.
Mahitaji ya huduma za kifedha hasa mikopo ni makubwa kuliko upatikanaji na huduma zenyewe. Ktk kila watu 100 wenye kuhitaji mikopo na huduma za kifedha ni watu 20 tu ndio wamefikiwa na huduma.

NB: Ni muhimu tukatambua soko huria ni ubepari na sifa kubwa ya kufanikiwa ktk ubepari ni kujua jinsi ya kuwanyonya wengine.
 
Back
Top Bottom