NMB yaja na Pesa Fasta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NMB yaja na Pesa Fasta

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by PayGod, Apr 22, 2011.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  BENKI ya NMB imezindua huduma mpya ya Pesa Fasta itakayomuwezesha mteja kuchukua fedha kwenye mashine za NMB popote bila kuwa na kadi wala akaunti.

  Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Mark Wiessing amezindua huduma hiyo leo Dar es Salaam na kuongeza kuwa, huduma hiyo ni rahisi , ya haraka na yenye kutoa suluhu la soko la huduma za kibenki.

  “Kufikia huduma za fedha ni moja ya changamoto ambayo wasimamizi wakuu kama BoT pamoja na benki nyingine kama NMB wanakabiliana nazo nchini pamoja na nchi nyingine,” alisema Wiessing.

  Amesema, kuzinduliwa kwa huduma ya Pesa Fasta itasaidia idadi kubwa ya Watanzania ambao hawakuwa na huduma za benki kupata huduma hizo ambapo kuanzia sasa watakuwa na upeo mkubwa wa kupokea fedha kupitia mashine za ATM za NMB.

  Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano cha NMB, Imani Kajula alisema faida za NMB Pesa Fasta haihitaji kuwa na akaunti, haihitaji kuwa na kadi ya NMB ATM, hakuna makato ya mwezi, mhusika anaweza kuchukua fedha kwenye ATM zaidi ya 400 na huduma hiyo inapatikana kwa saa 24.

  Amesema, jinsi ya kutuma fedha kutumia simu yako ya mkononi kwa huduma ya Pesa Fasta ni kupiga *150*66# na kisha kufuata maelekezo zaidi ambapo mteja anaweza kutuma au kupokea hadi Sh 200,000 kwa siku.

  Aidha, Kajula amesema, huduma hiyo pia itamwezesha mteja kuangalia salio, kutuma fedha kwenda kwenye akaunti ya NMB, kununua LUKU au muda wa maongezi au kupata taarifa fupi.
   
 2. Ally Msangi

  Ally Msangi Verified User

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Jun 29, 2010
  Messages: 580
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  hizo pesa unatoa vp kama huna akaunt number wala ATM card
   
 3. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ukiwa kwenye atm yoyote ya NMB BONYEZA TOP RIGHT HAND BUTTON, kisha fuata maelekezo, ambayo yatakuhitaji kuingiza namba mbili za siri na na kiasi ulichotumiwa, na utapata fedha yako
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  that means you must register for this service therefore there is nothing new .... just like m-pesa though the cash points are ATM'S ....isn't it ..?
   
 5. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  NMB PesaFasta Launch


  Today NMB has introduced NMB PesaFasta a new money transfer service that enables NMB mobile customers to send money to beneficiaries who don't have bank Account.NMB PesaFasta recipients will be able to withdraw transferred amount from NMB ATM anywhere in Tanzania. The launch of NMB PesaFasta is a continuation of NMB commitment in improving service delivery to customers
  [​IMG]NMB CEO Mark Wiessing unveiling NMB PesaFasta, with him (from right) is Financial Sector Deepening Trust (FSDT) Technical Director Sosthenis Kewe and NMB Head of Personal Banking Abdulmajid Nsekela.
  Speaking during the launch of NMB PesaFasta that was held in Dar es Salaam, NMB CEO Mark Wiessing said "NMB is delighted to announce the creation of NMB PesaFasta unique service which allows any NMB mobile customers to send money to beneficiaries who do not have yet a bank Account. This will allow these unbanked Tanzanians to start getting access to the normal banking system". [​IMG]  Financial Sector Deepening Trust (FSDT) Technical Director Sosthenis Kewe and NMB Relationship Manager Neema Kassim making transactions through NMB PesaFasta.
  Mr. Wiessing added "NMB PesaFasta is designed to be an affordable, reliable and convenient solution for our target market, including the so-called unbanked. A cheaper, better and faster money transfer service that uses NMB's leadership in technology".
  Speaking on behalf of NMB partners, Financial Sector Deepening Trust (FSDT) Technical Director Mr. Sosthenis Kewe, congratulated NMB for being a strong partner in bringing financial services to the unbanked.
  From now onwards you can access NMB PesaFasta service by dialing *150*66#
   
 6. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mtumaji lazima awe mteja wa NMB na ajisajili na nmb mobile ila mpokeaji anachotakiwa awe na simu ya mkononi tu.
   
 7. theophilius

  theophilius Senior Member

  #7
  Apr 22, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wangeshugulika kwanza na namna ya kupunguza msongamano kwenye benki zao, maana hii huduma kama inakuhitaji uende kwenye benk zao, utakuwa msalaba. kwa wanaojua hii benki wanajua ninachomaanisha. foleni kila mahali hata kujua salio, unakaa foleni masaa wee bila kuhudumiwa.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Anayetumiwa haitaji kujisajili, ila mtumaji lazima awe na akaunti ya nmb. Inabidi waboreshe atm mashine zao ili hii huduma iwe nzuri!
   
Loading...