NMB Public Share holding vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NMB Public Share holding vipi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lekanjobe Kubinika, Feb 26, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwaka na ushee umepita tangu kampeni ya kukusanya mitaji kwa ajili ya kuwekeza NMB umepita sasa, lakini kimya! Nakumbuka walikuwa wanadai wamekusanya kuzidi malengo na watawarudishia wengine pesa yao walioitoa kununua hisa za wananchi. Sijasikia kitu zaidi ya kusikia mamilioni ya pesa za NMB ama kuporwa au kupotea. Ule ulikuwa ufisadi kama DECI au? Ukiuliza watu wa NMB hawana maelezo yenye tija. Inaonekana hata wao hawajui.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Hivi hawa jamaa waliwahi kudeclare dividents maana yake naona kila leo wanagawa fedha tu leo shule hii kesho kule nchi nzima na hao viongozi wao inaelekea wanatumia hiyo nafasi kama campaign too for their political ambitions!! Kama mnazo kwanini hamtoi dividends kwa wanahisa? Mwenye taarifa tafadhali atumwagie kwanini hawagawi ingawa wanapata faida?
   
 3. e

  eddy JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2010
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 10,658
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  Dividend utaitoa wapi! akina Mengi umewaweka wapi (NICO)? togwa lishatiwa shubiri!
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Mengi anahusiana vipi na DIVIDEND policy ya NMB? Nadhani board ya wakurugenzi wa NMB ndio wanawajibika kwa hili!!
   
 5. D

  Donrich Senior Member

  #5
  Mar 12, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu Lekanjobe Kubinika na wengine,
  NMB baada ya kuuza hisa zake kwenye soko la msingi(primary market) through Initial Public Offer walizipeleka hisa kwenye soko la hisa la Dar-es-Salaam (secondary market).

  Kama unavyosema, ni kweli share zilikuwa oversubscribed,kwa hivyo walionunua hisa zaidi ya kiwango kilichotengwa walirudishiwa pesa zao,kumbuka kwenye Initial Public Offer kila hisa iliuzwa kwa shilingi 600,lakini ziliendelea kupanda bei mpaka ziliwahi kufika Tshs1200,ingawa baadae zilishuka mpaka kufikia Tsh730,nilipoangalia mara ya mwisho zilikuwa Tsh 830.

  Kuhusu gawio(Divident) walishawahi kutoa kila share Tsh30,kwa hiyo kwa ujumla NMB wanafanya vizuri kutokana na mwenendo wa soko la hisa la Dar-es-Salaam,nasema hivi kwa sababu ukilinganisha na hisa za CRDB ambayo toka hisa zimeingia sokoni hazijawahi kupanda hata siku moja na badala yake zimeendelea kushuka,ziliingia sokoni zikiwa Tsh200 kama sikosei ,lakini siku ya mwisho kuangalia zilikuwa zimeporomoka mpaka kufikia Tshs 130 kwa hisa ,na hawa wamewahi kutoa gawio ilikuwa shs 2 kila hisa.

  Kingine NMB kutoa misaada kwenye soka na sehemu nyingine siyo kuharibu pesa,isipokuwa hiyo ni corporate strategy ambapo inafaida nyingi,lakini nitataja mbili tu kwa sasa,

  1.Inacreate public awareness(kwa hiyo ni kama inafanya matangazo na promotion ya biashara hasa ukizingatia banking industry inaushindani mkubwa sana Tanzania at this particular momment).
  2.Inatimiza wajibu wake kwa jamii(Corporate social responsibility),kwa kuwarudishia kidogo kati ya michango yao mingi waliyoitoa kwa NMB kwa kufanya biashara nao,kama kufungua account,kuchukua mikopo, kusafirisha pesa nk
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Concern ilikuwa kwanini hawajagawa dividends toka miaka hiyo walipogawa hiyo shilingi 30 kwa share moja ingawa faida wanapata;wasingetoa misaada kama wasingekuwa wanatengeneza faida!!
   
 7. D

  Donrich Senior Member

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu Bulesi,NMB imeingia kwenye soko la hisa (Listing Date) tarehe 6/11/2008, na mwaka wake wa fedha unaisha kila tarehe 31,December ya kila mwaka.

  Kwa hivyo utaona kwamba mpaka sasa inamwaka mmoja tu na miezi kazaa katika soko la hisa,lakini wameweza kutoa gawio la Tsh 30 kwa kila hisa,mimi naona wamejitahidi sana,kumbuka kampuni inaweza kutoa gawio mara moja kwa mwaka au mara mbili kutegemeana na faida pamoja na mipango ya kampuni husika,ingawa sijui watatoa dividend nyingine lini,lakini naamini watafanya hivyo kabla mwaka huu haujaisha.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...