Nmb ni bank au? Tumeichoka sasa basi

Nmb ni bank au? Tumeichoka sasa basi

ABUMAN

Member
Joined
Dec 8, 2010
Posts
52
Reaction score
7
Habari wadau,Km mfanyakazi wa Serikali natoa hoja ya sisi wafanyakazi wa Serikalini tuhame kuitumia NMB kupitishia mishahara yetu kwani uongozi na wafanyakazi wameonesha kushindwa au kuzidiwa na kazi kiasi kwamba kuna baadhi ya wafanyakazi hasa wa tasnia ya Ualim wameshindwa kupata mishahara yao kwa muda sasa kwa kosa la hao wafanyakazi wa NMB wakati wa kuituma wanaituma kwa mtu mwengine na mtu anafuatilia miezi kadhaa anapewa ahadi tu na uongozi idara husika hawaoneshi ushirikiano wowote nina wasiwasi na taaluma ya watu wa idara husika kufuatilia wapi mshahara umeenda na kuomba uidhinishaji wa kuurudisha katika akaunti husika kuchukua miezi kadhaa kama ni hivyo hiyo idara iondoshwe wawe wanaomba watu waliobobea kutoka field husika yaani consultants wawasaidie kila mwisho wa mwezi au huenda wamezidiwa na kazi au wamewachoka wateja hasa wafanyakazi wa Serikali kutokana na wengi wao kupitishia mishahara NMB,naishauri kama si kuhama basi Serikali iwaache watu wachague Bank nyengine na mishahara iende huko moja kwa moja bila kupitia NMB wanachosha sana hawa jamaa hasa majibu na kiburi wanachoonesha.Nakusudia NMB Makao Makuu pale Phoenix House.
 
Ni kweli kabisa.
Nimejaza fomu za kufungua joint account mimi na mke wangu lakini leo ni mwezi wa pili naambiwa watu IT hawajaweza kutatua shida.
Pia hawana kauli nzuri na ya kumthamini mteja.
 
Weee bado uko kwenye hiyo benki ya Makabwelaaa? unafanya nn huko toka haraka.
 
Ni kweli kabisa.
Nimejaza fomu za kufungua joint account mimi na mke wangu lakini leo ni mwezi wa pili naambiwa watu IT hawajaweza kutatua shida.
Pia hawana kauli nzuri na ya kumthamini mteja.

Amen, usiwe na nyumba ndogo maana umejidhibiti hapo
 
Bank ya Makabwera, unategemea nini hapo, lazma mambo yaende kikabwela kabwela.
 
Huwa naifananisha na yale masoko ya mazao ya kulima!NMB SUCKS A LOT.
 
Ni kweli kabisa.
Nimejaza fomu za kufungua joint account mimi na mke wangu lakini leo ni mwezi wa pili naambiwa watu IT hawajaweza kutatua shida.
Pia hawana kauli nzuri na ya kumthamini mteja.

Si unajua mbongo akipata analewa ndo kama hivyo wamekuwa na wateja wengi na hawataki kuchukua hatua kwa ukuaji wao
 
Ni kweli kabisa.
Nimejaza fomu za kufungua joint account mimi na mke wangu lakini leo ni mwezi wa pili naambiwa watu IT hawajaweza kutatua shida.
Pia hawana kauli nzuri na ya kumthamini mteja.[/QU Unauweka usiku bure! Panga halikati mti mpaka nyuma liwe limeshikiliwa. Wanaona usomeki, utasuri sana.
 
Ni kweli kabisa.
Nimejaza fomu za kufungua joint account mimi na mke wangu lakini leo ni mwezi wa pili naambiwa watu IT hawajaweza kutatua shida.
Pia hawana kauli nzuri na ya kumthamini mteja.

polen sana. Bila kuandamana hamna majibu
 
Kwanini msifungue Akaunti NBC, MAHALA MTEJA NI MFALME? Polen sana watanzania.
 
Back
Top Bottom