NMB Idara ya mikopo Rushwa imekithiri


Kama sijakuelewa Mkuu!
 
Nilienda NMB pale Temeke Sudanese nikamkuta mama mmoja mweusi kibonge na yeye alinizungusha huyo wakati vigezo vyote nilikuwa navyo.Nikaenda zangu access bank na akiba commercial bank nikapata mkopo haraka na bila longo longo yeyote.
Yaani uhonge laki tatu ili upewe milioni moja dah kweli hawa hawana akili.
 

Umesoma vyema maelezo yangu? 🙁
 

Nashukuru kwa Ushauri mkuu.
 
Ndugu wana jamii forums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyiau chunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhari toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kamaifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 

Imenichanganya kuisoma habari hii kwa kweli, je ndio mtindo mpya wa kuandika huu kutoka bank au jina lako ni NMB
 

Sasa hapa ndo umeandika nini!!!!
Huo mshahara wanakulipa bure tu
 
Hata mimi nilizungushwa sana NMB-NELSON MANDELA MOSHI hadi basi kumbe jamaa anataka chake kwanza!
Kwa mil 6 alitaka 200,000, akaishia 150,000,hapo aligoma kabisa kushuka!
Nikakubali kitu kikatoka kimechomolewa 150,000.
UJAMAA na KUJITEGEMEA.
 
ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa.aliye kupa wewe ndie aliye wanyima.lakini ukumbuke mtaka chongo huita kengeza
 
mmeumbuliwa sasa naona mnatapatapa mchezo wenu kwishiney. mmeiba mno tena ninyi nisawa na vibaka mshahara unalipwa na benk bado tu pesa ya mtaja nayo uidandie.sijui mna mtindio wa ubongo
 
Ningekushauri umuone Meneja wa Tawi (Branch Manager) uwekano mkubwa hajui hayo matatizo unayopata kwa sababu moja ya lengo kubwa la benki ni kutoa mikopo na hilo lengo upewa Meneja wa benki kama kipimo chake katika kazi. unahangaika na watu wa chini ndio maana hupati jibu. huitaji kuhonga hata sumni, maranyingi wateja ndio uharibu wenyewe kwa kutoa hongo. unaombwa hela ya mfuta ya gari kwani ni polisi hao? gharama ya mkopo huwa inajumuisha yote hayo.
 
Matatizo ya rushwa kwenye mikopo sio NMB peke yako, karibu bank zote watu wanalalamika. Mkopo hausogei mpaka utoe ahadi ya kutoa kidogo kidogo kwa watakaokushughulikia, utadhani hawana mishahara wakati hizo ndio kazi zao. Stanbic, Standard chartered, Barclays na nyingine nyingine hali moja. Unawekewa vikwazo ambavyo havina maana ili mradi uwape chochote. EFC nao mpaka yule atakayeingiza file kwa boss kuidhinisha mkopo wako nae umpe chochote, vinginevyo file anatia kwenye draw yake linamaliza ma wiki halishughulikiwi. Upuuzi mtupu..! dawa ni kuwapa pesa ya PCCB au kuonana na boss mwenyewe ndio watatia akili. wanasahau kua wewe ndio utalipa mkopo na pesa nyingi unakatwa mwanzoni ambazo haziwahusu.
 
hiyo sio NMB tu asilimia kubwa ya bank za tz zinasumbua hivyo usumbufu kama huo nimejutana nao ACCESS BANK.
Nilipojaribu kugoma kutoa chochote kias walichitaka nikaambiwa siwez pata mkopo nilioomba bas ikabidi nitoe kias ili kupata mkopo kwa sababu nilikuwa na shida ndo maana nilitoa tena na hapo afisa mikopo kaniambia nimetoa ndogo kwa sababu haitoshi kugawana na bos wake kwa maana kuwa kuna mkubwa wake wa kaz wanakula nae deal hizo.
 
kumbe!! mimi pia yamenikuta nimejaza mkopo wiki inaisha sasa bado sijaingiziwa hela kwenye akaunti yangu... halafu naona kama afisa analeta ujanja ujanja kama ananisoma afanye kazi yake kabla sijaenda kwa meneja wake kumshtaki...
n.b SITOI HATA KUMI.
 
You can't be sereous mkuu unless we si mtanzania
 
msinikumbushe naweza kulia nmb nina viwango vyote vya rushwa 5m laki 4 10m laki saba utakiunaacha.
 
hua sitoi hata mia na mkopo napata kwa wakati.
 
Naona umeongea kama mmoja wa watu wapumbavu(hilo sio tusi). Hivi wewe unaelewa kweli maana ya National Microfinance bank?hivi do u know why NMB was formed from NBC? For your information ni kwamba kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogowadogo ndio lengo hasa la hiyo bank na wala sio watu wenye mitaj mikubwa kama unavyodhan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…