Mwandwanga
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 3,057
- 1,573
Nakushauri ukaelezee suala lako kwenye uongozi wa NMB uone watachukua hatua gani.
Laki tatu za nini!?
Kama ni kweli umefanya jambo zuri sana.
Wafanyakazi wengi kwenye maofisi ni warasimu sana kwenye utoaji huduma (rushwa ikiwa sehemu ya tatizo).
Sasa huyu anaomba mkopo wa 1m nayo wanaitolea macho!
Kuna faida kubwa sana kumhudumia mtu vizuri.Kuna mambo mengi sana unaweza kufaidika indirect. Imagine umemhudumia vizuri huyu mtu na kesho ukapita kwenye biashara yake iliyofanikiwa kwa mkopo huo..what a blessed your heart will be
Hili nilijaribu kwenda kwa Loan Manager ofisi yake inatazamana na ofisi ya huyu dada Elice. Nilipo mwambia suala la kuchelewa kujibiwa maombi yangu ya mkopo ili hali wana Hati yangu ya Nyumba! Alisema nirudi kwa Officer wangu.
Manager niliyemkuta ni mzee mweusi hivi ana lafudhi ya kinyakyusa.
Sidhani kama yeye ni wa mwisho kwenye Uongozi wa NMB.
wameomba laki tatu nenda kachukue moto takukuru uwapelekee waungue
mkopo wa milioni moja, mkopo wa laki tano unaenda bank ya NmB, duh, watanzania wana shidaaaaa, hiyo hela si ungekopa hata kwa rafiki yako tu jamani. pengine nmb wameona ni hasara, mikopo midogo hiyo hawawezi kukuthamini kwasababu una faida kidogo sana kwao ndio maana unaona kama wanakuonea. nenda saccos au upatu wa mtaani huko au weka hela kwenye kibubu, laki tano haustahili kwenda kukopa bank. tuache utani jamani. hata milioni moja au mbili unaenda bank? hizo hata waendesha bodaboda wanazo majumbani mwao, kwanini mnapenda kunia madogo kiasi hicho, think big, act big....alaaa.Naomba ushauri nifanyaje, hata kama wataninyima lakini niweze kutumbua jipu la urasimu huu.
Tawi la Kariakoo kuna jamaa anaitwa Julius
mkopo wa milioni moja, mkopo wa laki tano unaenda bank ya NmB, duh, watanzania wana shidaaaaa, hiyo hela si ungekopa hata kwa rafiki yako tu jamani. pengine nmb wameona ni hasara, mikopo midogo hiyo hawawezi kukuthamini kwasababu una faida kidogo sana kwao ndio maana unaona kama wanakuonea. nenda saccos au upatu wa mtaani huko au weka hela kwenye kibubu, laki tano haustahili kwenda kukopa bank. tuache utani jamani. hata milioni moja au mbili unaenda bank? hizo hata waendesha bodaboda wanazo majumbani mwao, kwanini mnapenda kunia madogo kiasi hicho, think big, act big....alaaa.
bank ya NMB nilipewa mkopo 15m rushwa nilitoa laki 5 ,
sasa nimeamua kuamishia majeshi bank ya post kule jamaa wako poa sana jamaa yangu kashepewa 10m na amewapa 40,000 tu
Sihitaji kuongopa Ndugu yangu.
Pesa ya mkopo ya awamu ya kwanza nili itumia kufungua mgahawa jirani na Chuo cha SAUT kampasi ya Mbeya.
Nilitoa rushwa kuanzia Bank mpaka ofisi za Halmashauri.
Sehemu niliyosaidiwa ni TRA na kwa Wanasheria tu.
Ingawa TRA ndio sehemu ambayo nilikuwa nimeitengea pesa ya kuhonga lakini hawakuomba hata senti moja.
Habari wana Ukumbi,
Leo nimekuja hapa barazani kufikisha kero yangu kwa benki ya NMB tawi la Mbalizi road MBEYA.
Mwaka 2013 mwezi wa Nne (04) nilienda kwenye ofisi zao, kwa minajili ya kuomba mkopo. Nilipofika pale nilikutana na Loan officer alijitambulisha kwa jina la Kirungeme.
Katika hatua za awali niliweza pata ushirikiano wa kutosha kwa huyu mfanyakazi. Nilipokamilisha hatua zote ikiwemo ile ya kuja kunitembelea na kuangalia shughuli zangu. Bank iliamua kunipa mkopo wa Tsh. 500,000/- ingawa niliomba Tsh. 1,000,000/-
Kadhia ilianza hapa;
Niliombwa pesa ya mafuta ya gari kwa kuja kunitembelea niliwapa 15,000/- (ilinibidi kutoa maana nilikuwa na shida hasa na ule mkopo)
Akanielekeza kwa mwanasheria atakaye gonga Muhuri na kunitajia kabisa kiwango cha kumlipa (niliambiwa nikamlipe 50,000/-) hili sikulifanya maana, nilienda States attorney nikapigiwa muhuri kwa 10,000/- na kuzirudisha form Bank. Nilipo zikabidhi form za mkopo kwa loan officer huyu alianza kugomba kwanini sijaenda kwa mwanasheria aliyenitajia!
Nilifanikiwa kuchukua mkopo, na kufanya marejesho kila mwezi kama mkataba wetu ulivyokuwa umeelekeza. Baada ya kukamilisha Marejesho, na kufanikiwa kulipa mkopo wote nilienda tena Bank n kukutana na Kirungeme akaniambia yeye kapanda cheo, ila atanikabidhi kwa Mtu mwingine.
Alinikabidhi kwa Mdada anaitwa Alice (ana asili ya kichaga) huyu dada ndio sababu hasa ya kuja kuomba ushauri hapa.
Nilimwambia nahitaji mkopo wa Tsh. 1,500,000/- nilifanya hivi kwakua lengo hasa nilitaka mkopo wa 1M lakini nilijua wanaweza punguza kama walivyonifanyia mwanzo hivyo nikaona niongeze hii 500,000/-
Huyu dada alinizungusha sana, kila nikimpigia simu waje kunitembelea alikuwa haishi Sababu. Nikajua ni walewale wanaohitaji RUSHWA nilimtumia Tsh. 25,000/- ilikuwa ni J3 hiyo siku, wakaja kunitembelea J5.
Kama kawaida akanielekeza kwa Mwanasheria , sikufanya hivyo tena, nikaenda States Attorney. Na huu mkopo nimeumaliza.
Sasa nilipotaka mkopo mwingine nikaona kama kuna kukwepana sana , nikamtuma MKE wangu, yeye ni mtumishi wa Umma. (Mwalimu) nikamwambia aende akope 2M.
Wameomba LAKI TATU ili waweze kutoa huu mkopo. Huyu dada anayeitwa Elice akiwa ni Mmoja wao.
Naomba ushauri Ndugu zangu.
Naomba kuwasilisha.