Nmb huduma kwa wateja tatizo nini??

Nmb huduma kwa wateja tatizo nini??

nanix

Senior Member
Joined
Oct 26, 2015
Posts
153
Reaction score
172
Kwa kweli leo nimefadhaika sana..nimetuma pesa kutoka nmb mobile kwenda mpesa jana usiku cha kushangaza mpaka hivi sasa haijafika kwenye mpesa yangu na kwenye akaunti ya nmb pesa imepungua nimewasiliana na vodacom wanasema pesa haijafika kwao.

Najaribu kuwapigia nmb huduma kwa wateja hawapokei haijawahi kunitokea kupiga simu huduma kwa wateja kwa masaa 12 non stop bila jibu lolote yaani muda wote hawapokei simu for the whole day nawekewa mziki tu mpaka nimeukariri wote na sauti inayosema simu yangu ni ya muhimu.

Hawajapokea simu mpaka hivi sasa nimefikiria namna ambayo naweza kupata msaada nikaona maybe jamiiforums naweza nikampata hata mfanyakazi mmoja wa nmb awashtue wenzake sababu haiwezekani ikawa kwamba wapo busy muda wote huo. Jamani nmb mnisaidie pesa ya mgonjwa hiyo inahitajika hospitali mnisaidie jamani..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wna thread jukwaa la HHM cheki nao
 
Back
Top Bottom