NMB hamtutendei haki wateja wenu

NMB hamtutendei haki wateja wenu

Dodoma moja

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
307
Reaction score
184
Wakuu ni wiki ya tatu hii tangu nilipoomba mkopo NMB lakini cha ajabu hakuna chochote hadi sasa kila nikienda naambiwa eti kuna matatizo ya mtandao kutokana na makao makuu kufanya marekebisho ya loan system hivyo mikopo yote imesitishwa hadi leo.

Sasa najiuliza je wanavyotufanyia ni haki maana hata malengo ya kukopa naona yanaanza kupotea kutokana na muda kuwa mrefu sana hadi nafikiria hata nihairishe.

Kwa mtindo huu CRDB watawapiga bao na hayo marekebisho yenu yasiyofika mwisho.
 
Hili ni la kweli nami nimeskia, ati pana maagizo kutoka juu makao makuu kutotoa mikopo mpaka mwezi Agosti tarehe haijulikani, labda maswala ya kutakatisha pesa wako ktk uchunguz
 
hli ni la kwel nam nmeskia, ati pana maagzo kutoka juu makao makuu kutotoa mikopo mpka mwez agosti tarehe haijulikani, labda maswala ya kutakatisha pesa wako ktk uchunguz

Yaani mkuu cha kusikitisha zaidi hata wahusika wa mikopo nao hawajui ni lini wataanza kutoa hiyo mikopo kila siku ukienda ni ahadi tu hadi kero!!!
 
hebu jaribu kuwachek makao makuu kwa cm usikie wanasemaje
 
wakuu ni wiki ya tatu hii tangu nilipoomba mkopo nmb lakini cha ajabu hakuna chochote hadi sasa kila nikienda naambiwa eti kuna matatizo ya mtandao kutokana na makao makuu kufanya marekebisho ya loan system hivyo mikopo yote imesitishwa hadi leo.

Sasa najiuliza je wanavyotufanyia ni haki maana hata malengo ya kukopa naona yanaanza kupotea kutokana na muda kuwa mrefu sana hadi nafikiria hata nihairishe.

Kwa mtindo huu crdb watawapiga bao na hayo marekebisho yenu yasiyofika mwisho.

na siku hizi wameanza upumbav mkubwa wa kulazimisha watumishi wapitishie mishahara kwao ndipo watoe mkopo,wakati siku za awali haikuwa sharti,bravo crdb maana kufungua akaunti ni siku moja tu na wako innovative
 
Mimi sitaki hata kuisikia NMB. Niliweka Fixd Acount ya Miezi sita. Mpaka leo ni Miezi Tisa Inafika kila nikienda Nazungushwa tu. Mara nenda bank house mara nenda tawi la temeke ni usumbufu tu jaman. Pesa yangu mwenyewe lkn inanitesa mpaka najuta na hii bank jaman. Nadaiwa kodi na fees za wanangu
 
Back
Top Bottom