Nkurunziza: Nitalipiza Kisasi

Nkurunziza: Nitalipiza Kisasi

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,511
Reaction score
53,474
150515034200_burundi4_624x351_afp_nocredit.jpg

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewapongeza wanajeshi wazalendo waliozuia mapinduzi na kurejesha hali ya usalama na utawala huru mjini Bujumbura.

Rais Nkurunziza amewataka waburundi wazalendo kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi utakaofanyika mwezi juni.

Rais huyo alikuwa Mjini Dar es Salaam Tanzania siku ya Jumatano kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kundi la wanajeshi waasi walipotangaza ''Mapinduzi'' dhidi ya serikali yake.

Viongozi watatu miongoni mwa makamanda6 wa jeshi waliounga mkono tangazo hilo la ''mapinduzi'' ilikupinga muhula wa tatu wa rais huyo tayari wamekamatwa.
Kufikia sasa watu 105,000 wameripotiwa kutorokea mataifa jirani kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Baada ya kurejea kutoka Tanzania rais Nkurunzinza alielekea Kaskazini mwa Bujumbura eneo alikotokea kabla ya kurejea katika kasri la rais lililoko katika mji mkuu wa Bujumbura.

Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni rais Nkurunzinza alisema kuwa ''

kuna amani na utangamano katika asilimia kubwa ya Burundi na hata katika mji mkuu wa Bujumbura ila tu watu wachache waasi ndio waliokuwa na hamu ya kuvuja damu''
''Jeshi la taifa lilionesha ukomavu wake lilipokabiliana na wasaliti hao''

''Ningependa kuwahimiza waburundi wazalendo walinde kwa dhati amani iliyoko sasa kwani ndio ngao na msingi wa demkrasia iliyoko Burundi''

''Shari msingi wa demokrasia yetu changa ilindwe isiyeyuke''

Nkurunziza aliahidi kulipiza kisasi dhidi ya ''yeyote aliyejaribu kuwasha moto wa uhasama baina ya waburundi''

Rais Nkurunzinza aliwasili mjini Bujumbura Ijumaa akiwa ameambatana na maelfu ya wafuasi wake.

Wengi wao wafuasi wa chama chake ambao walimshangilia kwa kurejea kwake huko .
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema japo asilimia kubwa ya mji huo ulikuwa na amani, katika sehemu zingine kulikuwa na waandamanaji walioweka vizuizi barabrani wakipinga kuwania kwake kwa muhula wa tatu.

Polisi wa kupambana na ghasia walikuwa wakikabiliana nao kwa kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi.

Miongoni mwa makamanda waliokamatwa kwa kuchochea uasi ni pamoja na waziri wa zamani wa ulinzi Cyrille Ndayirukiye.

Waziri wa sasa wa usalama Gabriel Nizigama aliiambia BBC kuwa maafisa wawili wakuu katika idara ya polisi pia walikamatwa pamoja na wadogo wao takriban 12 waliokuwa wakiwalinda.

Wawili hao walikamatwa baada ya ufyatulianaji wa risasi nje ya jumba walimokuwa.
Kiongozi wa uasi huo meja jenerali Godefroid Niyombare,aliyetangaza ''mapinduzi'' hayo siku ya jumatano hajakamatwa japo alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema kuwa atajisalimisha.

''Nitajisalimisha kwa utawala, natumai hawataniua'' alisema meja jenerali Niyombare.

Chanzo: BBC
 
Katika mazingira ya sintofahamu ambapo hata yeye hajui nani ni nani, sikutegemea ataanza kuwabeza wapinduzi kwamba ndio wanataka kuvuja damu.

Sifahamu ni kwa nin anatangaza kulipa kisasi katika nchi ambayo raia mamilioni wanakimbilia uhamishoni, taasisi nyingi za juu wanampinga na jeshi limegawanyika.

Katika hali ya kawaida, ilitosha kuona kwamba warundi hawamtaki kwa kuangalia maelfu wanaoandamana kumpinga, maelfu waliongia barabarani kushangilia alipopinduliwa wakiwa tayari kutoa ushirikiano kwa serikali mpya ya kijeshi!.

Maelfu hao waliingia barabarani wakitembea sambamba na askari wamapinduzi kuashiria wallikuwa tayari kushirikiana na serikali yoyote ambayo ingeundwa kutoakana na hayo mapinduzi. Wapinduzi wake walikuwa wastaarabu, hawakumwaga damu na walilinda raia.

Akili ya kawaida ilitosha kumwonyesha hapendwi kwa kuangalia tu kwamba maelfu wameshangilia kupinduliwa kwake, lakini aliporudi, mamia tu ndio waliingia kumpokea.

Badala ya kutangaza vifo vya kisasi, alitakiwa aonyeshe kuwa logical kwa kuwaunganisha Warundi, kuwashawishi kwamb lolote analolifanya hata huko kuvunja katiba ni kwa ajli ya Warundi. Vinginevyo anajiandaa kutawala kidictator sasa anataka kuwa terrorize watu wamwache afanye atako au waface kifo.

Na hapo awe na mtazamo mpana wa kulia na kushoto kwa sababu anazidi kujiwekea maadui na wanafiki wengi.
 
Haya ndio madhara ya kufata ushauri wa wajinga!!nilisema siku ile humu ndani kwamba Niyombare anachuki binafsi na Pierre kwasababu ya kufukuzwa kwenye idara ya kijasusi na wala hana uzalendo na burundi!

Ona sasa alivyowatesa wenzie na yeye kukimbia.
 
Akifanya hivyo atakuwa anakosea sana.

hawezi akaacha kutoa vitisho wakati akitazama kisogoni anaona tsunami ya vitisho nyuma yake! warundi wana hasira naye sana analijuwa hilo, nchi kaiharibu katika kila jambo ... ndio maana akawaomba FDRL watoe mafunzo kwa Imbonerakure(Interahamwe Burundian version) ufichoni ndani DRC kusudi litakalo kuwa na liwe, luckily those concerned are watching closely, remember #neveragain ?
 
Haya ndio madhara ya kufata ushauri wa wajinga!!nilisema siku ile humu ndani kwamba Niyombare anachuki binafsi na Pierre kwasababu ya kufukuzwa kwenye idara ya kijasusi na wala hana uzalendo na burundi!

Ona sasa alivyowatesa wenzie na yeye kukimbia.
Kimbley;
Kwa hiyo weye unashauri kwamba Pierre amnyonge hadharani?? Pierre ana haki gani ya kuwatawala watu wasio mtaka? Siku zote uelewe, ukiwatawala wasio kutaka, hutalala usingizi kamwe.
Si ninasikia kuwa huyo Pierre ni Mlokole au ni maneno tu. Lazima aelewe kuwa neno la Mungu linasema kuwa kisasi ni cha Mungu wala sisi tusilipize kisasi. Amshukuru Mungu kuwa amemrudishia madaraka wala hakumpa mamlaka ya kuua.
Tena neno linasema; Adui mpende wala sio umuue. Weye nnani unamwua mwenzio? Waangalie wauaji, hawana mwisho mwema. Kwani lazima ung'ang'anie haya madaraka? Hawaoni kina Generali Obasanjo. Wanaheshimika kila mahali
 
ukisema hivyo utakuwa unakosea! jamaa alikuwa ashaona Nkurunziza hana support kutoka kwa wananchi sema mahesabu yake hayakuwa kama ya General wakweli... utawezaje kutangaza coup détat wkati bado haujadhibiti vitu vyote vya muhimu? lakini kuhusu support wote tuliona jinsi wananchi wa lika na jinsia zote walivyofurahi na kuingia barabarani tofauti na Nkurunziza aliyekuja kupokelewa na maelfu ya vijana(Imbonerakure) peke yake
 
sasa unakataa nini unakubali nini
 
sasa unakataa nini unakubali nini

kuna usicho elewa? nasema sio chuki binafsi!!! jamaa alikuwa kashaona jamaa wananchi hawamtaki ndio maana akachukua maamuzi ya harakaharaka kabla hata ya kuwatuliza wapambe wa Nkurunziza wote bila kusahau na Imbonerakure zilizolipiza kisasi cha kuchoma radio za waandamanaji... understand?
 
Kimbley;
Kwa hiyo weye unashauri kwamba Pierre amnyonge hadharani?? Pierre ana haki gani ya kuwatawala watu wasio mtaka? Siku zote uelewe, ukiwatawala wasio kutaka, hutalala usingizi kamwe.
Si ninasikia kuwa huyo Pierre ni Mlokole au ni maneno tu. Lazima aelewe kuwa neno la Mungu linasema kuwa kisasi ni cha Mungu wala sisi tusilipize kisasi. Amshukuru Mungu kuwa amemrudishia madaraka wala hakumpa mamlaka ya kuua.
Tena neno linasema; Adui mpende wala sio umuue. Weye nnani unamwua mwenzio? Waangalie wauaji, hawana mwisho mwema. Kwani lazima ung'ang'anie haya madaraka? Hawaoni kina Generali Obasanjo. Wanaheshimika kila mahali

Mimi simtetei Pierre naomba uelewe!hivi mnafahamu huu mzozo chanzo chake jamani??Pierre kosa alilolifanya ni kubadili katiba na kujihalalishia kugombea tena kwa mara ya tatu!!na sio kutawala tena kimabavu kama ulivyozungumza!

Warundi walikuwa na haki ya kumkataa PIERRE kwenye box ya kupigia kura,ijapokuwa sipingi maandamano yao.

Unajua kwanini Niyombare alipelekwa kenya kama balozi?na unajua kwanini Niyombare alifukuzwa kwenye idara ya ujasusi burundi miezi mitatu iliyopita?
Halafu hakuna sehemu nimeiunga mkono au kukubali kwamba PIERRE amuue Niyombare.
 
something fish! yaani nkurunziza kapinduliwa mara mapinduzi yamezimwa! kirahisi rahisi tu kama sinema,nitaamini huu ujinga pale nitakapo muona nkurunzinza ndani ya bujumbura akihutubia wananchi.
 
hebu wacha kupoteza wakati kama mambo hauyajuwi!!! jamaa alipigwa chini na baadaye kidogo habari ika leak, upo hapo? tatizo lilikuwa ni kwamba, alimtuma kumfanyia uchunguzi ya jinsi wananchi wanavyo mwona! jamaa akaenda akamtengenezea report ya kurasa 15 ambayo inasema chama chao kiko popular sana na kitachaguliwa kwa asilimia kubwa nchini Burundi lakini endapo Nkurunziza atakuwa sio candidate kwa mara ya tatu, siunajuwa tena waafrika hatupendi kuambiwa ukweli mchungu? hapo ndio jamaa akaanza kumuona nuksi na kumfuta kazi!
 
kama hii comment kama ni ya kwangu basi ngoja nijibu na kama hainihusu niambie
 
Bora hata angesema sheria ichukue mkondo wake, badala ya mikwara ya kisasi. Huyu jamaa naona hajui Warundi kweli wamechoka naye na anataka kusababisha vurugu mbaya sana. Wengine hata mishipa inawatoka kwa hamaki.
1508080_921232444605611_4335632953078893921_n.jpg
Jamaa kashajipatia Boss Tangawizi mishipa inataka kuchana ngozi!!
 
hawezi akaacha kutoa vitisho wakati akitazama kisogoni anaona tsunami ya vitisho nyuma yake! warundi wana hasira naye sana analijuwa hilo, nchi kaiharibu katika kila jambo ... ndio maana akawaomba FDRL watoe mafunzo kwa Imbonerakure(Interahamwe Burundian version) ufichoni ndani DRC kusudi litakalo kuwa na liwe, luckily those concerned are watching closely, remember #neveragain ?
Naona unaendeleza chukizako, tupe link inayo wahusisha FDRL kutoa mafunzo Chambawima1 sikuzote huwa una chuki lakin kama NKURUNZINZA atafanya kulipiza basi atakuwa kaiga kwa KAGAME, na itakuwa ni tatizo kwa Burundi kuwa na amani jMali nikweli FDRL wanahusika?
 
Last edited by a moderator:
Acha mbwembwe wewe Box la kura co ishu...mtu anaweza kuiba kura atakavyo na hata akishindwa hang'oki....King'ang"anizi haondolewi kwa box la kura
 
Waafrica tunamawazo finyu sana kwani nchi nzima aliumbwa aongoze yeye milele

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Acha mbwembwe wewe Box la kura co ishu...mtu anaweza kuiba kura atakavyo na hata akishindwa hang'oki....King'ang"anizi haondolewi kwa box la kura
yani kama vile CCM mfano wa karibu kabla sijaenda mbali
 
Back
Top Bottom