Nkamia songa mbele zaidi na hoja yako uitendee haki na ututendee haki wote

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,725
2,000
Kwa muda mrefu sasa Nkamia amekuwa akizungumza ndani na nje ya Bunge kuhusu kuondelewa kwa ukomo wa madaraka, vyovyote vile iwe kwa wabunge au rais.

Kila mara ukimsikiliza anaamini kwamba uchaguzi wa mara kwa mara na ukomo wa madaraka sio kigezo cha maendeleo na rejea zake ni kwa Ujerumani na Rwanda.

Nkamia na wenzake watujibu haya; Je kutukuwepo kwa ukomo wa madaraka ndio kielelezo cha demokrasia na maendeleo? Je US kwa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka 4 kwa rais wake na na ukomo wa madaraka imeifanya nchi yao kuwa maskini? Ni kweli hajui kuwa Ujerumani ina Rais ambaye ana ukomo wa madaraka?

Ni kweli tumefikia hatua ya kujifunza kwa nchi kama Rwanda iliyojengwa kwa matumizi mazuri ya misaada ya 'mabeberu' na wizi wa rasimali Congo? Kama ameweza kufananisha Messi kuendelea kucheza tu mradi yuko katika kiwango bora, anaweza kufananisha hivyo pia kuuvunja mkataba kabla ya muda wake kuisha pale ambapo kiwango kimeshuka?

Mh.Nkamia usiishie tu kutuambia uchaguzi na ukomo wa madaraka sio kigezo cha maendeleo, maana utaambiwa pia mataifa vituko na yaliyojichokea kama Equatorial Guinea, Uganda, Zimbabwe, Sudan, Cameroon, Gabon hayana ukomo wa madaraka na ni mafukara wa kutupwa pamoja na rasimali walizonazo.

Nenda mbali zaidi kwa kutupa sababu za kuchukia ukomo wa madaraka na pia kutaka kuongezewa muda wa kukaa madarakani zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom