Nkamia azomewa Jimboni kwake

Nkamia azomewa Jimboni kwake

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,710
Reaction score
3,685
Katika hali inayoonyesha kubanwa na kupata upinzani mkubwa ndani ya chama chake cha CCM,mbunge wa Chemba Juma Nkamia,amejikuta akizomewa na wananchi wake wakati wa kujinadi kuomba kura za kuteuliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo kupitia CCM.

Nkamia alijikuta ktk hali ngumu baada ya kupanda jukwaani ili kuomba ridhaa ya wanachama kumchagua kwa mara nyingine kupeperusha bendera ya chama,kundi la vijana lilikatiza hotuba yake kwa kupiga kelele na kumzomea kuwa ashuke jukwaani kwani hakuna kitu alichokifanya kwa kipindi cha miaka mitano zaidi ya porojo ndani ya bunge.

"Sema ulichotufanyia kwenye ubunge wako wa miaka mitano,hatutaki upoteze muda,hapa tuna migogoro ya ardhi,shida ya maji,huduma mbovu za afya,elezea umefanyaje ili serikali itatue?".Hata hivyo Nkamia akaishia kusema tu wananchi wakasome vipeperushi vyake alivyogawa watajua nini kafanya.

Akijibu swali la kuzuia mauwaji mpakani mwa Chemba na Kiteto,Mh. Nkamia alisema ya aliwaamuru wananchi wa Chemba wakapambane na wafugaji,na walifanikiwa na kuanza kulima..hali hii ilimfurahisha Rais Kikwete mpaka akamteua kuwa Naibu Waziri wa Habari,Michezo na Utamaduni.

Hali imezidi kuwa mbaya kwa mbunge huyo ndani ya hekaheka za kula za maoni.
 
Kati ya wabunge wenye kibri wa CCM huyu anaongoza, hebu mchinjieni bahari kuu na damu isionekane kama alivyofanywa Osama na Marekani
 
Zomea kabisa mzee wa ndiyoooo. Kila kitu ndioooo ulifikir wananch wako hawakuoni sasa utavuna ulichopanda
 
Mi nasema hafai na atoke maana hakuna namna tumemchoka sasa aende huko TBC awe co wao.
 
huyu nkamia mjinga sana bungeni boraa Kibajaji kuliko huyu.Wananchi zomea tu ata mawe na fimbo apigwe
 
Yaani huyu jamaa huwa simpendi tu
sijui kwa sababu gani...
 
Apigwe tu namimi nasema apigwr tu arushiwe mawe tu maana tumechoka sasa na dioooooooo. Azomewe tuu.
 
Duh afadhali yamemkuta aliyostahili huyu baradhuli mkubwa akafie mbali.
 
Nkamia ni miongoni mwa wanaojipendekeka au kujikomba kwa wakubwa ili wapate vyeo. Na wanavipata kweli hasa kwa wakubwa na maboss wa Kitanzania, kama Magufuri, Mwigulu nk. Lakini ni chukizo kwa jamii. Mara nyingi kauli zao ni za maudhi na kutaka sifa, huwa hawajisimamii kama Deo Filikunjobe au Lugola
 
Kiburi si maungwana. Amejisahau maana alidhani miaka mitano ni mingi sana. Anaona tabu gani kuwaeleza wananchi alichokifanya mpaka awaamuru wakasome vipeperushi vyake?
 
Dawa ya moto ni moto, shika kadi yako futa, ondoa, delete, kata, sambaratisha ccm
 
Back
Top Bottom