Njooni tutete

charrote

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Posts
1,988
Reaction score
4,413
Habari ya uzima,

Naomba niwasilishe hoja yangu kama ifuatavyo...

Nakumbuka nikiwa shule ya msingi darasa la sita ndipo yale masomo ya ukuaji wa binaadamu ndipo yalianza kuzungumzwa kwa upana katika somo la Sayansi. Nikiwa sekondari mada za ukuaji na mahusiano ya kimapenzi mpaka kufikia kuzaliana zilikua zikifundishwa kwa upana sana.

Kadri unavyoendelea kuongeza elimu unaweza kugundua kuwa suala zima la mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume ni muhimu sana. Hata tukirejea katika maandiko matakatifu wakati wa uumbaji Mwenyezi Mungu baada ya kumuumba Adam(mwanaume) akaona si vyema awe peke yake hivyo hakumuacha peke yake akamletea msaidizi Eva (mwanamke).

Naomba tujadiliane kwa kina suala hili kwa upande wa ndugu zetu walioko magerezani(wafungwa). Je kuwa mfungwa tayari unakuwa umepoteza haki yako ya kuwa na mwenza wako kama ilivyoagizwa na Muumba?

Kwanini usiwekwe utaratibu walau mara moja kwa mwezi na wao waweze kutendea haki hisia zao? Ikiwa wewe huwezi kumaliza wiki bila kushiriki mapenzi inakuwaje kwa mwenzio ambaye anatumikia kifungo miaka 25 au maisha yote? Au kuna kipengele katika katiba kinakataza? Kwanini?

Mwenye majibu anakaribishwa.
 
Hayo masomo ya ukuaji nikiyakumbuka huwa napata hasira sana coz ndio yalisababish niijue punyeto kipindi cha darasa la sita.

Kwa nchi yetu hapa nashisi ukishakuwa mfungwa tu haki zako nyingi za msingi unazikosa ikiwepo hiyo ya kuwa na mwenza. Ndio maana inasemekana huko magerezani kuna tabia za usodoma na ugomora kwa wale wenye nguvu zaidi.
 
Mkuu niliona kwenye prison break jamaa walikuwa jela ila wakawa wanaruhusiwa kuonana na wapenzi wao kila baada ya muda mpenzi au mke wake anakuja na kumpa papuchi.
Nadhani mataifa mengine wanaruhusu hili.
 
Mkuu niliona kwenye prison break jamaa walikuwa jela ila wakawa wanaruhusiwa kuonana na wapenzi wao kila baada ya muda mpenzi au mke wake anakuja na kumpa papuchi.
Nadhani mataifa mengine wanaruhusu hili.
Kwa hapa kwetu Tanzania Kuna utaratibu gani?
 
Ndio maana Wafungwa wanyonge wanageuzwa Wanawake ndani ya Magereza...

Ni shirika la haki za binaadamu pekee, linalo weza kupendekeza hili katika tawala zilizo Madarakani, kubadili hali.

Lazima Serikali itambue, wahanga wa kwanza katika hili ni wafungwa chini ya 20 na wale wanyonge wasio himili Mikiki ya Jela..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli ni jambo dogo lakini lina maana kubwa inabidi tupate pá kusemea
 
Nchi za wenzetu kuna utaratibu wa wafungwa kuonana na wapenzi wao private. Huku kwetu sijui
 


hahahaha duh darasa la 6?hahahh
 
Kwa hapa bongo wanashogoana na kusagana kumaliza au punyeto inahusika hakuna namna na huwezi kuzuia hili, kwa upande wa wadada nadhan askar huwapunguzia hasa wenye shape nzuri
 
Kwa hapa bongo wanashogoana na kusagana kumaliza au punyeto inahusika hakuna namna na huwezi kuzuia hili, kwa upande wa wadada nadhan askar huwapunguzia hasa wenye shape nzuri
 
Sex ni haki ya msingi aliiweka mwenyezi Mungu alipomuumba Eva ili wawe wawili. Wafungwa ni haki yao kuwe na mpango wa kuwakutanisha na wenzi wao angalau mara moja kwa mwezi. Kama kiongozi mhusika ni mcha Mungu afikirie swala hilo. Pata kila kitu hata uwe tajiri ukose hiyo haki huna raha, unateseka kisaikologia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabisa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…