Njooni huku Boko Mnemela viwanja vya bure

Range rover

Senior Member
Nov 22, 2016
186
195
Wadau hamjambo?

Nimehamia huku panaitwa Zumba mabanzini mkoa wa Pwani, kwa ufupi unapo toka Dar panda magari pale Mbezi yanayokwenda Boko Mnemela ukifika Boko Mnemela kodi boda boda elfu 6 mpaka huku Mabanzini.

LIFE YA HUKU
Huku wamang'ati bado wapo wamezuia maeneo, yaani nilichofanya nimemuhamisha mmang'ati kwa laki 8 eneo la heka 9

Bado bushi sema kanisa katoliki wamekuja juzi nao wanajenga hostel za masister na ndio wanafanya harakati za kuweka umeme.

Life ya huku ni ya ki nzuri maeneo mengi ni msitu na serikali imeweka bango ukisafusha eneo ndio lako nyumba ni chache ila vibanda vya wamang'ati na mashamba ya mahindi tu ndio mengi.

Yaani kwamimi niliekulia tarangire hapa nnahisi kama nipo home aisee ni kuzuri tambarare yake usipime huku watu wengi wafugaji, kuku, nguruwe, mbuzi, kilimo cha karanga, matikiti, mahindi, pilipili mwendo kasi, maziwa ya ng'ombe kwa wingi naona watu hawaja pastukia this gift land.

Karibuni sana
Mabanzini, Zumba
 
Asante kwa taarifa

Vipi lakini mlipiga kura kuchagua mwenyekiti wa mtaa? au mnaishi kienyeji tu.
 
kuna maeneo ya mohamed huko, watu wamelia sana huko kuna kipindi eka ilikuwa inauzwa 50000/=tsh
 
Naomba tofauti ya :-

1. wamangati

2. wahandzabe

3. wabarbaig

4. watindiga
 
Range rover naona watu wanakudhihaki lakini hawaoni mbali.
Miaka ya nyuma viwanja vilikuwa vinatolewa Madale ya Mivumoni kwa 20k, niliona ni ujinga nani aende porini lkn leo hugusi kiwanja pale.
Ukiona kanisa Katoliki wametia timu hapo patamu, hawa ni wazee wa maono wanaona mbali, soon wanajenga chuo, hospitali nk.
Nitakucheki mkuu
 
Ukinitajia maeneo hayo namkumbuka mtaalamu mzee nyoka kala sana hela za mashamba alikuwa ana tukusanya kwake Enzi zile 2011 mna fanya mikutano ya viwanja


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom