Njoo tuelekezane jinsi ya kupiga hela Burundi

Jembebutu

Member
Feb 14, 2017
88
225
Ndugu zangu kuna biashara nataka kujaribu kufanya ya kutoa bidhaa Kariakoo kupeleka Burundi ila katika pitapita, nimegundua changamoto zifuatazo.

1. Mabadiko ya thamani ya pesa ya Burundi
2. Ugumu wa kubadilisha fedha. Yaani ukiwa na faranga ni ngumu sana kuirudisha kuwa Shilingi.
3. Suala la usalama hasa unapokuwa na cash.

Naomba msaada kwa Mrundi au Mtanzania mwenye uzoefu au uelewa kwenye hayo masuala. Napenda kujua tofauti ya thamani ya fedha zetu pia bidhaa zenye uhitaji mkubwa Burundi zinazopatikana Bongo.

Shukran sana.
 
Sasa mkuu watu wanafanya biashara mashariki mwa Congo, ambako hata bank ni shida, sembuse Burundi, ambako bank zipo?
Hapo cha kufanya ni hizo pesa za Burundi unakwenda sehemu za kubadilishia(bank) kwani Burundi kwenye kubadilisha pesa ni wakali sana, wanataka uende sehemu rasmi, tatizo lao sasa ni rate za chini sana!!!

Utapata dola,
 
Hivi CRDB bado iko Burundi au ndio ilishakufa?
 
Hivi CRDB bado iko Burundi au ndio ilishakufa?
CRDB ipo bado lkn pia KCB ipo vile vile changamoto benki ya taifa (BRB) imezuia miamala ya kimataifa kwa sarafu ya BIF (faranga)

Hivyo ili ufanye miamala kimataifa ukiwa Burundi unatakiwa uwe na akaunti ya dola CRDB wanayo na KCB pia wanayo, ukiwa Burundi unaweza kudepost na kuwithdraw kwa dola kupitia akaunti yako hiyo hiyo hiyo.
 
Ni kwel mimi ninafanya biashara huko simu zinauzika sana wao wanatumia sana itel hata smart zao nyingi ni itel changamoto ni mfumo wa chaja kule hawatumii chaja kama zetu ukimuuliza huyo rafiki yako atakuambia vizuri kwa kukushauri kama una mtaji mzuri unaweza kufungua kabisa duka lako kule ukaweka mtu wako akakuuzia, au wewe mwenyewe ukabaki kuwa unaagiza tu bidhaa zinakukuta kule.
 
We upo sehem gani Bujumbura or
 
Mkuu naomba namba yako kama hutojali. Au unaweza kunicheck tuyajenge kaka 0756981717
 
Wanatumia cable za matundu mawili au?

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Wanaogopa kutakatisha pesa
 
CRDB Bank wana tawi Burundi. Jaribu kupata taarifa kama unaweza kuhamisha faranga kwenda Tsh na vice versa.

Kuhusu ujambazi inategemeana na mitaa unayopiga mishe na kuishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…