Njoo hapa tufundishane na tusaidiane jinsi ya kuishi na mke kwa akili

Kuna ule usemi maarufu unaosema "wanaume ishini na wake zenu kwa akili"

Lakini wengi hawajui maana halisi ya huu usemi,

Leo nitakufundisha maana ya huu usemi kwa mifano halafu utakwenda kujiongeza kwa mkeo.

1. Mkataze mkeo jambo kwa kumzunguka (kwa akili)

Kwa mfano, umerudi nyumbani unakuta mkeo anaongea ongea na kwa wakati huo wewe hutaki kelele

badala ya kumwambia funga mdomo wako, mwambie mke wangu ukifunga mdomo wako lips zako zinapendeza sana.

Kwa akili za wanawake atanyamaza tu, hapo utakuwa umemkataza jambo kwa akili.


2. Jambo la kawaida lifanye kuwa special kwake.

Kwa mfano. Umepata mchongo wa pesa.

Badala ya kumwambia mke wangu kuna mchongo wa pesa nimepata,

Mwambie mke wangu kuna siri nataka nikwambie, hiyo siri sijamwambia yeyote yule.

Atakuuliza siri gani hiyo, hapo ndo utamwambia kuwa kuna mchongo wa pesa umepata na hili jambo hata ndugu zangu sijawaambia.

Kwa akili za wanawake atajiona mtu special sana na ataona unamjali sana maana jambo umeshindwa kuwaambia ndugu zako lakini yeye umemwambia, lakini nyuma ya panzia labda ndugu zako umeshawaambia


3. Muombe ushauri hata katika mambo ambayo huhitaji ushauri wake.

Kwa mfano, mtu mzima umejichanga changa unataka kununua gari, na ushafanya utafiti gari gani itakufaa kutokana na pesa uliyonayo.

Sasa badala ya kumwambia mke wangu nataka kununua gari,

Mwambie mke wangu nina mpango wa kununua gari, naomba ushauri wako gari gani itatufaa.

Kitendo hicho kitamfanya mkeo ajione na yeye ajione mtu katika watu. Kwa sababu hakuna kitu wanawake wanapenda kama kushirikishwa katika maamuzi hata kama kwa unafiki.


4. Yapambe mapungufu yake.

Kwa mfano mkeo ni flat screen (hana mkia), sasa siku umemtoa zako out halaf akapita mwanamke anabonge la shepu.

Usiache hiyo fursa ikupite, huo ndo muda wa kupamsifia mkeo ili na yeye ajione mtu kwenye watu,

Mwambie mkeo ujue mijanamke yenye makalio makubwa hainaga akili, na utaweka mbwembwe nyingine nyingi


Hapo mkeo utamteka akili maana udhaifu wake umeupamba kwa kuukandia uzuri wa mwanamke mwengine


5. Mtafutie sababu ya kumuomba msamaha

Hakuna kitu mwanamke anafarijika kama kuombwa msamaha na mumewe.

Sasa mwanaume inabidi sometime umkosee mkeo kwa makusudi ili upate sababu ya kumuomba msamaha.

Kwa mfano, siku unaweza kurudi nyumban ukamnunia tu bila ya sababu.

Halaf asubuh ukamwambia mke wangu nisamehe sana Jana nilikununia bila ya sababu.

Kitendo cha wewe kumzoesha kumuomba msamaha mara kwa mara atajiona mtu katika watu. maana ni wanaume wachache sana wenye tabia za kuwaomba msamaha wake zao.




Kama kuna tukio lolote ulishawahi kulisolve kwa akili share na sisi.

Na kama kuna tatizo lolote na mkeo unataka tukusaidie kulisolve kwa akili share hapa wadau wakupe mawazo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,

"wanaume ishini na wake zenu kwa akili" siyo usemi, ni andiko la kwenye Biblia Takatifu (1Petro 3:7)-"Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili....".
 
Katika kuishi nae kwa akili, pesa haihusiki? Au hapo kila mtu atajiongeza kivyake?!
 
Back
Top Bottom