Njoo hapa tufundishane na tusaidiane jinsi ya kuishi na mke kwa akili

Jaalut

Member
Jan 18, 2020
72
244
Kuna ule usemi maarufu unaosema "wanaume ishini na wake zenu kwa akili"

Lakini wengi hawajui maana halisi ya huu usemi,

Leo nitakufundisha maana ya huu usemi kwa mifano halafu utakwenda kujiongeza kwa mkeo.

1. Mkataze mkeo jambo kwa kumzunguka (kwa akili)

Kwa mfano, umerudi nyumbani unakuta mkeo anaongea ongea na kwa wakati huo wewe hutaki kelele

badala ya kumwambia funga mdomo wako, mwambie mke wangu ukifunga mdomo wako lips zako zinapendeza sana.

Kwa akili za wanawake atanyamaza tu, hapo utakuwa umemkataza jambo kwa akili.


2. Jambo la kawaida lifanye kuwa special kwake.

Kwa mfano. Umepata mchongo wa pesa.

Badala ya kumwambia mke wangu kuna mchongo wa pesa nimepata,

Mwambie mke wangu kuna siri nataka nikwambie, hiyo siri sijamwambia yeyote yule.

Atakuuliza siri gani hiyo, hapo ndo utamwambia kuwa kuna mchongo wa pesa umepata na hili jambo hata ndugu zangu sijawaambia.

Kwa akili za wanawake atajiona mtu special sana na ataona unamjali sana maana jambo umeshindwa kuwaambia ndugu zako lakini yeye umemwambia, lakini nyuma ya panzia labda ndugu zako umeshawaambia


3. Muombe ushauri hata katika mambo ambayo huhitaji ushauri wake.

Kwa mfano, mtu mzima umejichanga changa unataka kununua gari, na ushafanya utafiti gari gani itakufaa kutokana na pesa uliyonayo.

Sasa badala ya kumwambia mke wangu nataka kununua gari,

Mwambie mke wangu nina mpango wa kununua gari, naomba ushauri wako gari gani itatufaa.

Kitendo hicho kitamfanya mkeo ajione na yeye ajione mtu katika watu. Kwa sababu hakuna kitu wanawake wanapenda kama kushirikishwa katika maamuzi hata kama kwa unafiki.


4. Yapambe mapungufu yake.

Kwa mfano mkeo ni flat screen (hana mkia), sasa siku umemtoa zako out halaf akapita mwanamke anabonge la shepu.

Usiache hiyo fursa ikupite, huo ndo muda wa kupamsifia mkeo ili na yeye ajione mtu kwenye watu,

Mwambie mkeo ujue mijanamke yenye makalio makubwa hainaga akili, na utaweka mbwembwe nyingine nyingi


Hapo mkeo utamteka akili maana udhaifu wake umeupamba kwa kuukandia uzuri wa mwanamke mwengine


5. Mtafutie sababu ya kumuomba msamaha

Hakuna kitu mwanamke anafarijika kama kuombwa msamaha na mumewe.

Sasa mwanaume inabidi sometime umkosee mkeo kwa makusudi ili upate sababu ya kumuomba msamaha.

Kwa mfano, siku unaweza kurudi nyumban ukamnunia tu bila ya sababu.

Halaf asubuh ukamwambia mke wangu nisamehe sana Jana nilikununia bila ya sababu.

Kitendo cha wewe kumzoesha kumuomba msamaha mara kwa mara atajiona mtu katika watu. maana ni wanaume wachache sana wenye tabia za kuwaomba msamaha wake zao.




Kama kuna tukio lolote ulishawahi kulisolve kwa akili share na sisi.

Na kama kuna tatizo lolote na mkeo unataka tukusaidie kulisolve kwa akili share hapa wadau wakupe mawazo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi sijajaliwa hayo yote!

Na hapo ndio nahisi wataliwa kimasihara mpaka mkome!! Unambembeleza?

Mwanaume maneno mawili tuu! yakizidi sana matatu unaenda kazini..hivyo hivyo ukirudi,ubaya ukimzoea sana anakuona kama fala/bwege lake au huna lolote

Na tukizinguana mimi dk moja sio nyingi nimeshamfokea,akirudisha hovyo..kofi la maana! Habari imeisha..baadae kdg tunacheka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia mshirikishe katika matumizi ya pesa yako, mfano mahitaji ya nyumbani unaweza ukampa hela akanunua yeye na si wewe kuleta kila kitu. Kwa kufanya hivyo atajiona ana mamlaka katika nyumba
 
Uzi mzuri sana,
Ila nashauri kuwa mbabe kwanza ili ajue UKALI wako.Kisha anza ku-aplly mbinu hizi!!

When your toddler was learning to walk, you’d encourage her to get back up after she fell down,Parents should practice that approach as their children get older.
 
Mwambie kuna simu kali unataka kumnunulia inauzwa milioni na laki mbili,kwahiyo akupe pesa yake ya upatu laki 5 wewe utajazia laki 7,akitoa laki tano unaenda kumnunulia simu hiyo hiyo la laki 5


Sent using IPhone X
 
Uko sahihi japo hawa viumbe hawana kanuni,hawatabiriki! Huyu akiwa hivi mwingine ni tofauti..kuna factor nyingi zinazoweza kumfanya awe hivyo alivyo!
 
Mwendo ni kuwa mgumu kama chuma cha pua..pesa na show za kibabe..kuwa mkali na makini kwenye mambo yako..acha masihara na maisha..make no excuse kwenye mission zako.
 
Back
Top Bottom