Njia zitumikazo kusambaza taarifa za uzushi

1701075383223.jpeg
Usambazaji wa taarifa potofu umekuwapo muda mrefu sana, usambazi wa taarifa potofu umekuwa ukifanywa kupitia njia mbalimbali kama;

Mitandao ya Kijamii
Mitandao ya kijamii imekuwa ni njia ya haraka na inayoweza kufikia watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi, hii imekuwa ni moja kuu ya kusambaza habari.

Kupitia njia hii watu waovu wamekuwa wakiitumia kusambaza habari potofu kwa manufaa yao. Wamekuwa wakitumia majukwaa kama Facebook, Twitter, WhatsApp, na Instagram kusambaza habari za uwongo au uzushi.

Barua pepe na Ujumbe
Njia hii imekuwa ikitumiwa kwa muda mrefu kusambaza jumbe za uongo, mara nyingi imetumiwa a matapeli kuibia watu.

Watu wamekuwa wakitumiwa barua pepe zenye jumbe zushi za kulaghai huku zikiwataka wasambaza zaidi ili washinde zawadi kitu ambacho ni uongo.

Blogs, Tovuti na chaneli
Watu wamekuwa wakiandika machapisho ya blogu au kuchapisha habari za uwongo kwenye tovuti zao, na kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii au kwa kutumia viungo au chanel zao kama Youtube.

Ushiriki (utiririshaji) wa Moja kwa Moja (Live Streaming)
Katika zama hizi, uzushi pia huenezwa kwa kufanya matangazo ya moja kwa moja (live streaming) kwenye majukwaa ya video kama vile YouTube, Facebook Live, au Twitchnk, watu wasio na nia njema hutumia njia hizi kueneza uzushi na kukika matumizi mazuri ya majukwaa haya.

Kupitia Mikutano na Matukio ya mikusanyiko
Wakati mwingine, watu wenye nia mbaya wanaweza kutumia mikutano au matukio kama vile mikutano ya umma au mikutano ya kisiasa kusambaza habari za uwongo.

Uwapo kweye moja ya majukwaa hayo au mikutano ni vyema kuchuja na kufanya uhakiki wa kila unachokutana nacho au kukisikia.

Ana kwa ana
Kupitia mazungumzo ya ana kwa ana mtu mmoja kwenda kwa mwingine huweza kusambaza taarifa potofu, iwapo mtu anayezungumza naye aidha ana nia ovu ya kukupotosha au naye alisikia taarifa potofu na hakuihakiki anaweza kukwambia kilichopotofu na akakupotosha iwapo nawe utaamini bila kuhakiki.

Unaweza kuhakiki habari kupitia majukwaa ya uhakiki kama hili la Jamiicheck ili kupata uhakika wa maudhui uliyosikia au kusoma.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom