Njia za wizi zinazotumiwa na Makampuni Bandarini

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Baada ya CAG kufanya uchunguzi na Mapitio ya matumizi ya mafuta ya msamaha katika kampuni za madini yalionyesha kuwa kampuni mbili za Geita Gold Mines na Resolute Tanzania Limited, zilihamisha mafuta ya msamaha kwa kampuni nyingine zisizo na misamaha hiyo. Jumla ya thamani ya mafuta yaliyokuwa na msamaha wa kodi ya TZS. 22,325,178,728 yalihamishwa ambapo TZS. 22,305,069,488 yanahusu Geita Gold Mines Ltd na TZS. 20,109,240 yanahusu Resolute Tanzania Limited.

Uhamishwaji wa mafuta hayo kwenda kwa kampuni isiyo na misamaha hiyo ni kinyume na tangazo la serikali Na. 480 lililochapishwa tarehe 25 Oktoba, 2002. Tangazo hili la serikali linataka kusitishwa kwa misamaha kama mafuta ya msamaha yatatolewa kwa matumizi mengine au kuhamishwa, kuuzwa au kutolewa kwa namna yoyote ile kwa mtu asiyestahili misamaha hiyo.

Baada ya kugundua wizi huu, ofisi ya CAG ilipendekeza;
kwa menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kurejesha kodi ya mafuta yanayosafirishwa kwa wakandarasi waliopewa kazi na mkandarasi mkuu ya kiasi cha TZS.22,305,069,488 kwa M/s Geita Gold Mines na TZS.20,109,240 kwa Resolute Tanzania Limited, na M/s Geita Gold Mines Ltd.

Matokeo:
Hakuna lililofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Geita Gold Mines and Resolute Tanzania Limited wameendelea kudunda mitaani pamoja na kuiba pesa za Watanzania TZS 22,325,178,728.

Hizi pesa kama zingekusanywa zingenunulia vitanda vya wagonjwa vingapi?

Kweli Tanzania ilikuwa ni shamba la bibi!
 
Sasa naanza kuelewa kwa nini Kikwete alikuwa na mtandao mpana namna ile wakati wa juhudi zake kuwa raisi. Ingawa kura alipewa na watanzania maskini, lakini yeye aliingia kwa ajili ya kazi moja tu ya kupiga hela pamoja na makampuni washirika wake. RIP Ally Zona, kijana aliyeuwawa wakati Kikwete anatumia dola kulazimisha kubakia madarakani. Sababu halisi ni hii ya kupiga ufisadi wa namna hii. Hakuna mjinga au lofa atakayeamini kuwa Kikwete alikuwa hajui haya mambo au hakushirikishwa...
Rais wangu JPM sasa tumbua majipu papa, haya majipu dagaa yaliyokuwa yanaamrishwa achana nayo, tumbua muamrishaji
 
Duh! Yaani hii nchi kila unakogeuka ufisadi tu. Jamani tuanzishe sheria za kunyonga wahujumu uchumi.
 
Back
Top Bottom