Njia ya ukamilifu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,826
730,260
Ndani ya ukristo tunaambiwa kuwa chini ya jua hakuna mkamilifu la hata mmoja kwakuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.. Neno wote wametenda dhambi Pengine ni ile dhambi ya asili pale Eden kwakuwa kiimani sisi sote ni uzao wa Adam na Eva.

Tukiachana na imani ya kikristo na sect zake unapokuja kwenye imani zile zinazoabudu miungu(masanamu) wao wanaamini kwamba kupitia mafunzo sahihi basi mmoja anaweza kufikia utimilifu kamili na hata kuwa mungu kama vile yule mtoto wa mfalme tajiri aliyeacha kila kitu na kwenda kutafuta chanzo asili na ukweli wa mateso ya binadamu na viumbe hai.

Sakyamuni/Saidharta Goutama Buddha
Ndani ya Buddhism ukifuata mfumo huu unaweza kufikia utimilifu.


--mtazamo sahihi
--dhamira sahihi
--lugha sahihi
--matendo sahihi
--maisha sahihi
--juhudi sahihi
--tafakuri sahihi
--fikra sahihi

Kwa ujumla wake haya yote mtu akiyatenda kwa asilimia mia moja huyo ni mkamilifu.... Lakini cha kujiuliza ni wangapi walau wameweza kufikia asilimia 70?
Hii ni tafakari ya Jumatatu ngoja nikuachie uitafakari hata katika maisha yetu ya kila siku bila Kuwa na dhana yoyote ya kiimani

Jr.
 
Bwana Yesu akubariki mkuu Mshana
img_3058.jpg
 
Back
Top Bottom