Diesel generator
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 706
- 663
Biblia inaeleza yusufu aliuzwa na ndugu zake na akapitia shida, tabu, utumwa, kifungo gerezani. Badae ndie alikuja komboa watu wa taifa lake dhidi ya njaa ugenini baada Mungu kumuinua. Tundu lisu alipigwa risasi, ikabidi aondoke nchini, akatibiwa Kenya, Mungu akamuinua raisi kenyata kumpa ulinzi wa kijeshi mgonjwa hospital!! Tena mgonjwa toka taifa jirani!!. Pamoja na kuwa mbunge, na taifa lake kugoma kumlipia matibabu!! Bado Mungu aliinua watu kumhudumia!!. Mungu kwa uwezo Wake kainua watu tena wakampeleka ubeligiji!! Mungu kamsimamia kapona. Njia za mungu azielezeki,. Waliompiga naamini wanajuta !!. Kumbe walikuwa wanamtengea njia ya kwenda kuonana na wafadhili kwa mudá wa kutosha bila halaka na kuweza kuongea nao kwa upana. Mliona wandishi wa kimataifa na viongozi wa ulaya walivyopishana kumjulia hali na kufanya maongezi. Na matokeo tunayaona sasa!! Tunaumiza vichwa!!. Njia za mungu hazielezeki!!. Huu ni mwanzo na tusipomludia Mungu tukaungama yatatufika makubwa zaidi. Namtizama lisu kama kiongozi wa Mungu alie hai. Kwanza hana kashfa za ovyo, kwa wanawake umsikii, ufisadi hayumo, sio mnafiki. Risasi na mtililiko Wake adi kupona!! Hakika mkono wa Mungu uu juu yake. Endeleeni kushupaza shingo, zitavunjika ghafla.