Njia ya Kurudisha Ubira wa Elimu

Njia ya Kurudisha Ubira wa Elimu

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Wadau leo nimeona niongelee kidogo changamoto za Elimu hapa nchini. Tumeshuhudia Serikali ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana na changamoto za kielimu hususani mapungufu yanayojitokeza katika baadhi ya Taasisi hapa nchini. Baadhi ya Taasisi hizo zimepewa adhabu kama kuzuiliwa kudahili wanafunzi na nyingine kufungiwa. Hatua hizi zimechukuliwa dhidi ya Taasisi hizo kwani zimeshindwa kukidhi baadhi ya vigezo muhimu kama vile kukosa wataalamu wenye sifa stahiki,vitendea kazi stahiki,baadhi ya Taasisi kutoa G.P.A kubwa kuliko uwezo wa wanafunzi, kudahili wanafunzi wasio na sifa n.k. pamoja na matatizo mengine lukuki.
Nimeona kuwa katika kudhibiti changamoto hizo kwanini Serikali isifanye maamuzi ya kuvunja baadhi ya Taasisi hizo za Elimu na kuziweka kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam? Zipo sababu za nyingi kwanini Taasisi hizo ziwekwe nchini ya Chuo Kikuu cha Dar es salaa ikiwemo historia iliyotukuka ya chuo hicho,ubora wa Elimu inayotolewa,vitendea kazi vya uhakika,mfumo mzuri wa kupata wanataaluma chuoni hapo,miundo mbinunk. Aidha twajua kabisa hata katika ushindani kimataifa chuo hicho kimeendelea kufanya vema kulinganisha na vyuo vingine.
Naamini kuziweka Taasisi hizo nchini ya Chuo Kikuu Dar salaam kutaondoa kama sio kumaliza matatizo hayo yaliyopo Taasisi hizo za Elimu. Kwa kuongezea hata utoaji wa G.P.A kwa chuo hicho unazingatia uwezo halisi wa mwanafuzi tofauti na sehemu nyingine.
Kwa kuanzia napendekeza Taasisi zifuatazo zivunjwe na bafala yake ziwekwe nchini ya Chuo Kikuu Dar es salaam.
a) Chuo Kikuu Dodoma
b) Chuo Kikuu Mzumbe
c) CBE
Naomba kuwasilisha.
Boniphace.
 
Weka herufi "k" kwenye neno ubira ili ueleweke.
 
Heading tu utata sasa sizani kama hiyo njia itapatikana
 
Back
Top Bottom