Njia ya kupata amani ya kweli duniani hii hapa

Njia ya kupata amani ya kweli duniani hii hapa

Mfalme Ahmad

Member
Joined
Nov 30, 2014
Posts
12
Reaction score
0
Hakuna kitu chenye thamani kama maisha ya upendo na amani. Kila mtu anatamani apate amani ya kweli katika maisha yake ya kila siku. Ni jambo la kumshukuru mungu kwamba nchi yetu sio miongoni mwa nchi ambazo zina machafuko na vita japo hatuwezi kutabiri maisha ya baadae. Tunapaswa kumuomba mungu atusaidie katika hili

Katika dunia ya leo kuna silaha za aina nyingi sana na za kisasa ambazo zinaweza kuangangamiza watu na mali zao kwa muda mfupi kabisa. Mfano wa silaha hizo ni pamoja na silaha za nyuklia, silaha za kibiologia na makombora na mabomu ya kila aina. Kuna bunduki pia ambazo ndizo zinazotumika katika vita ya aridhini.

Kazi ya silaha ni kuuwa na kudhuru, kazi ya silaha ni kuharibu. Hatuwezi kujisifia kwamba kuwa na silaha za kisasa ni maendeleo kwa mwanadamu labda huwa ni maendeleo kwa watu na serikali ambazo hupenda kutumia mabavu kuhakikisha kwamba matakwa yao yana adhiri watu wengine kwa nguvu.

Silaha yaweza kutumika katika kukandamiza watu na kuwanyima uhuru. hapa itabidi silaha zitumike kuondoa tabaka la wakandamizaji na kuleta tabaka lenye kujali utu. Silaha zaweza kutumika katika kulinda uhuru uliopatikana dhidi ya wakara ambao hupenda kuingiliana au kuhusiana na watu wengine ki mabavu

Kuna Jambo ambalo huwa linaniumiza kichwa sana hasa ni kiwaza kwamba silaha hizi zipo kwa ajili ya kuuwa na kutisha wanadamu. mtu akitaka kuuwa tembo atahitaji bunduki. Gobole linatosha kabisa katika kumuua tembo au mnyama yoyote yule wa mwituni. Kwa hiyo basi maendeleo katika nyanja ya silaha ni kwa ajili ya kuua watu wengi kwa mkupuo mmoja na kuharibu mali na kuwarudisha nyuma kimaendeleo watu wa jamii iliyopigwa na silaha hizo.

Watu wa zamani pia walikuwa wanapigana vita. Lakini vita yao ilikuwa ya mapanga na mishale. Walikuwa wanakufa watu ambao wamejitokeza kwenye uwanja wa vita tu na madhara yake kwa jamii husika hayadumu kwa muda mrefu kwa sababu silaha zao zilikuwa hazina uwezo wa kuharibu miundo mbinu ya jamii. Vita vilikuwa ni vya wanaume

Jambo ambalo limekuwa likiniumiza kichwa ni kwamba kama kuuwa tembo unahitaji gobole tu au mtego, Hivi huyu mwanadamu amefanya uhalifu gani mpaka astahili silaha nzito kama za nyuklia na mabomu ya kila aina?

Adui wa amani yetu kwa jamii ya sasa ni silaha zilizopo. Kwa mfano marekani ipata raisi mpenda vita kama bushi na akapata mpinzani mwenye nguvu kama urusi basi silaha za nyuklia zinaweze kuangamiza viumbe hai wa dunia ya leo

Kimefika kipindi cha wanadamu wote kuungana na kupaza sauti zao kupinga uwepo wa silaha kubwa na kulinda amani yetu iliyopo

Sasa ni wakati wa kushinikiza mataifa yote yawe na msimamo mmoja wa kuharibu silaha zote nzito na kuzika elimu na technologia ya kuzitengeneza. Na watu waache kujifunza sanaa ya vita. kwa njia hii amani ya kweli itapatikana

Vile vile duniani kusiwepo wanajeshi bali askari tu ambao watakuwa wamepata mafunzo na mazoezi ya kuwa na nguvu na uwezo wa kupigana kushinda raia wa kawaida. Hata bunduki pia sio silaha nzuri.


by King Ahmad.

Mimi ndio yule mfalme (mpakwa mafuta) ambaye atasimamia amani na utajiri wa dunia. Hibu fikiri endapo nitaleta usawa na kisha kufuta silaha, maisha yatakuwaje? Wanyama porini ni madui kati ya jamii moja na nyingine lakini kwa binadamu adui yake ni mwanadamu mwenzake. Wanadamu wakipatana maisha yatakuwa mazuri ajabu. Sema hapana kwa vita na umaskini. Mfuate mfalme.... Fuata Nuru

"watu hawata jifunza sanaa ya vita na watafua panga zao kuwa majembe na mikuki yao kuwa miundu

Nimeanzisha group la whatsapp liitwalo Kingdom of The Earth KTE. tuma namba yako kwenda 0688795814 ni ku add
 
Back
Top Bottom