Njia ulotupitisha CCM lazima turudi tulikotoka kabla ya Kufika Tunakokwenda

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,452
3,065
Ni kweli kuwa TANU na CCM zimesaidia sana kutupatia mafanikio ambayo tunayo kama yapo; Ni kweli kwamba uongozi wa Mwl Nyerere umetusaidia sana TZ kujenga nchi na huruka ya wananchi wake. Hongera CCM ya Mwalimu.

Kwa mpenda maendeleo ambaye pia ni mwanachama wa CCM kama ambavyo wengi wa watanzania waliwahi kuwa wana TANU au CCM, ni wazi ili kuondoka hapa tulipofika, ambayo si sehemu mbaya japo sio sehemu tuliyotaka kwenda tunahitaji wanaCCM wengi kuachana na CCM na kuungana na mbadala wa CCM ili wote kwa pamoja tufike tulikotaka kwenda. Hii hatua ni lazima, maana tumekwama lazima tujaribu mbinu nyingine za kujikwamua- Shime wanaCCM rudisheni kadi zenu kisha mchukue kadi mbadala kwa manufaa ya taifa lenu. UOGA ndo adui mkubwa ya maendeleo, acheni uoga ktk kusimamia taifa.

Nadhani furaha ya kufika kwenye mafanikio, kwenye taifa linalojitegemea ni furaha ya taifa; CCM wamejaribu bila mafanikio. Nachokili kuwa wamefanikiwa ni kuonesha kuwa kwa mbinu na uongozi wao taifa lolote haliwezi kufikia maendeleo yanayo kusudiwa. Hongereni kwa kuonesha mbinu ambazo haziwezi kunufaisha taifa.

Shime watanzania, tuungane kurekebisha makosa; moja, kwa kuwapumzisha CCM ili tushinde; ni kama kwenye mpira substitution huwanyika ili kufanikisha lengo la mchezo ambao mara nyingi ni kushinda; pili, faida ya CCM kumpuzika ni ya taifa zima, hivyo waone furaha kubwa kupumzika. Pumzikeni kwa furaha na amani kwamba, watanzania wenzenu pia wanaweza kuongoza ili kuona kama tunaweza kujikwamua na umaskini wa taifa tajiri kama letu; PUMZIKA KIKWETE, PUMZIKA MSEKWA, PUMZIKA PINDA, PUMZIKA SHEIN, PUMZIKA CCM. Pole kwa kazi ngumu ambayo haikuzaa matunda, umejaribu kwa kiasi chako. ACHENI CCM IFE, ili TAIFA LISIFE, hamna cha kupoteza maana TAIFA litabaki.

Ushauri wangu kwa CCM na WanaCCM, Tanzania.
 
Unawaudhi sana CCM, lakini hii ni mojawapo ya njia rahisi kwao. Ilibidi wakati wa kuingia vyama vingi, CCM isiruhusiwe kuendelea kuwepo, hila nalo ni kosa lililofanyika.
 
Kaa la moto like this this post. No more comment.
BUT itakuwaje wakikataa kujipunzisha???
 
Uwezo wa kufanya maamuzi ambayo binafsi huyapendi kwa manufaa ya UMMA; huo ndo uongozi; Kweli CCM wasingependa chama kife (wanachama 4milions maana 5mil haiwezekani CDM imewapunguza sana mwaka huu), lakini kwa manufaa ya watanzania 40milions plus.

Kwani Katiba ya CCM haina sehemu inaeleza jinsi chama kinavyoweza kufa?? watumie kipengere hicho kujifuta kwenye siasa za tanzania kwa manufaa ya taifa.
 
Binadamu ni kiumbe ambaye kwa huruka anapenda kumwamini binadamu mwenzake "trusting creature". Imani hiyo hupotea kabla ya binadamu kuacha kumwamini tena binadamu mwenzake. CCM mliaminiwa bila hata ya jasho, kwa kuzaliwa kwetu na huruka yetu tu tuliwaamini, sasa hatuwaamini tena kwa fedha, tisheti, kanga this time hata mtoe pajama kwa wamama na wababa imani imekwisha. mbaya zaidi it is not renewable imani, it is gone by the wind nobody can run after it, it is gone.

Imani tuliyoigawa kwa CCM kama njugu maji; sasa gharama yake haiwezi kulipwa na CCM wala mwanaccm; Tunaikabidhi kwa mdau mwingine ili afanye tunavyokubaliana kwa manufaa ya wote, akishindwa tutampa mwingine tena na wala sio CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom