Njia sahihi ya kupata asilimia ya kura za urais Zanzibar, Jecha yuko sahihi?

Aug 19, 2015
48
29
Kawaida asilimia ya kura huwa inatazamwa toka kura halali (VALID VOTES) na si kura zilizopigwa(TOTAL VOTES) . Maana yake ni kwamba Dr Shein ana kura 299,982 Kati ya kura halali 328,327(valid votes) na si 299,982 kati ya kura 341,865(total votes) kwasababu asilimia inatafutwa toka kwenye Valid votes na si TOTAL VOTES. Lowassa alikuwa sahihi sana kusisitiza hawa jamaa kupata ELIMU maana wanapotoshwa na kazi ya ni COPY&Paste bila kufikiri na kuchambua, Tufanye hesabu kidogo hapa

Ukichukua kura alizopata Shein ambazo ni 299,982 kati ya 328,327 unapata kweli amepata asilimia 91.366839% ambazo ukifanya makadirio ya kimahesabu unapata 91.4%

Nafahamu kuna watakaobisha ngoja niwarudishe kidogo kwenye matokeo ya Urais wa Tanzania Oktoba 2015 ili tupate reference nzuri,

Magufuli alipata kura 8,882,935 ya kura halali(Valid Votes) 15,193,862 hivyo kupata asilimia 58.46%. Kwa maana nyingine kama ingekuwa asilimia inatafutwa kwa kupitia (Total votes) ambazo ni 15,589,639 basi Magufuli angepata 56.9% ya Total Votes ambazo zilikuwa ni 15,589,639

ELIMU ELIMU ELIMU
 
Huyu Malisa hutowa chambuzi potofu mara nyingi...huwa nakosoa..lakini ili kumsaidia na kuongeza weledi kwa chadema wajaribu kumuonya manake hii ina akisi uwezo wa chama na wanachama wa chadema katika uchambuzi wa mambo ya kimsingi...alishawahi kuja na uchambuzi wa takwimu kiuchumi kuhusu bei ya bidhaa na nilihofu ikitokea ingetafsiriwa kiingereza tungepata aibu kama taifa....!
 
Unajaribu kusema Nini Mkuu? Au ndo mambo ya shibe haya, mchana huu!
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu. Kulikuwa na thread humu imetupofoa wote tusiojua tofauti kati ya kura halali (VALID VOTES) na kura zilizopigwa(TOTAL VOTES).

Nadhani mhusika ataiona hii thread !
 
Huyu Malisa hutowa chambuzi potofu mara nyingi...huwa nakosoa..lakini ili kumsaidia na kuongeza weledi kwa chadema wajaribu kumuonya manake hii ina akisi uwezo wa chama na wanachama wa chadema katika uchambuzi wa mambo ya kimsingi...alishawahi kuja na uchambuzi wa takwimu kiuchumi kuhusu bei ya bidhaa na nilihofu ikitokea ingetafsiriwa kiingereza tungepata aibu kama taifa....!

Kwa fikra zako, basi itakuwa ina akisi uwezo wa Watanzania kwa ujumla ......................!!!
 
Kawaida asilimia ya kura huwa inatazamwa toka kura halali (VALID VOTES) na si kura zilizopigwa(TOTAL VOTES) . Maana yake ni kwamba Dr Shein ana kura 299,982 Kati ya kura halali 328,327(valid votes) na si 299,982 kati ya kura 341,865(total votes) kwasababu asilimia inatafutwa toka kwenye Valid votes na si TOTAL VOTES. Lowassa alikuwa sahihi sana kusisitiza hawa jamaa kupata ELIMU maana wanapotoshwa na kazi ya ni COPY&Paste bila kufikiri na kuchambua, Tufanye hesabu kidogo hapa

Ukichukua kura alizopata Shein ambazo ni 299,982 kati ya 328,327 unapata kweli amepata asilimia 91.366839% ambazo ukifanya makadirio ya kimahesabu unapata 91.4%

Nafahamu kuna watakaobisha ngoja niwarudishe kidogo kwenye matokeo ya Urais wa Tanzania Oktoba 2015 ili tupate reference nzuri,

Magufuli alipata kura 8,882,935 ya kura halali(Valid Votes) 15,193,862 hivyo kupata asilimia 58.46%. Kwa maana nyingine kama ingekuwa asilimia inatafutwa kwa kupitia (Total votes) ambazo ni 15,589,639 basi Magufuli angepata 56.9% ya Total Votes ambazo zilikuwa ni 15,589,639

ELIMU ELIMU ELIMU
Jaribu kuwa mstaarabu kidogo
 
Back
Top Bottom