Njia rahisi ya kuondokana na yanayojiri katika Bunge letu tukufu

kampelewele

JF-Expert Member
Oct 13, 2014
2,963
2,346
Salaam wanabodi,

Kwanza kabisa tukumbuke kuwa Wabunge ni wawakilishi wa wananchi wa jimbo husika. wawe wamemchagua au hawakumchagua ili mradi ametangazwa kuwa ni mbunge wa jimbo fulani, anakuwa ni mbunge wa eneo hilo.

Kiini cha mgongano kati Bunge letu mara kwa mara ni wabunge kujifungamanisha na vyama vyao. Siamini katika Tanzania yetu kuna majimbo tawala wala ya upinzani. Na kama wabunge ni wawakilishi wetu kwa nini waitwe wa CCM au wa Upinzani? Ingekuwa vyema kama masuala ya vyama yakaachwa nje ya Bunge nao wakiingia Bungeni wanakuwa ni wawakilishi wa wananchi. Hata mkao lazima wakae alfabetikale tu.

Napendekeza katiba tuliyonayo iwekwe kiraka ili:-
1. Mbunge au kiongozi yeyote akichaguliwa awe ni mwakilishi wa watu wote, hivyo hata chama kikichukua kadi yake yeye aendelee kuwa mbunge wa jimbo husika na awe na hiari ya kuhamia chama anachotaka bila kuathiri ubunge wake. Hii itaondoa hofu ya wabunge wetu kufukuzwa chama na kukosa ubunge, hivyo watakuwa ni wawakilishi wa wanajimbo baadala ya sasa kuwakilisha vyama
2. Mgombea binafsi aruhusiwe kikatiba
3. Waziri asiwe mbunge wa jimbo

Nawasilisha kwa maoni ya ziada
 
Back
Top Bottom