Muendelezo....
Kwenye kila hustle huwa kuna vikeazo vyake , Baada ha kuelezea mawazo yangu juu ya namna mtu anaweza hamia Australia wacha niongelee niliyosikia kwa upande wa Spain.
Yafuatayo Ni maelezo pia niliyopata toka kwa mtu ambaye rafiki yake alishatumia hiyo njia. Ni Mtu wa Morocco ambaye sasahivi amebakiza muda mchache apate Residentship ya Spain.
Kuna njia inaitwa “Arraigo Social” unaweza itafiti zaidi. Hii imekaa hivi: kama unataka kufika Spain itakubidi ucheze na VISA yeyote ile either Tourist Visa au Esucation Visa , hii inakubidi uwe na senti kidogo na wengine hutafuta admission za vyuo na kulipia kiasi kama nusu semester n.k nia ni kupata visa tu.
Baada ya hapo ukishapata nafasi ha kuingia Spain sasa unakua mchakarikaji unatafuta kazi za kufanya na kazi ni nyingi ila za kawaida na pia kama una qualifications nzuri hnaweza bahatisha kazi nzuri. Sasa hapo inategemea kama utaweza kuendelea kusoma sawa kama utataka kufanya kazi tu sawa. Na pia ni vema kabla ya kutumbukia Spain uwe na ka connection ka kuanzia pamoja na Vihela kiasi (fanya research).
Then baada ya hapo unaweza ku overstay na kutafuta kazi , hio ni hata baada ya visa yako kuisha unaendelea kupambana na hakuna bugudha sana kama nchi zingine (kwa maelezo aliyonipa) , kwa upande wa Tourist visa ambayo huwa mara nyingi haizidi miezi Mi3 inakupa kipindi cha hiyo miezi mi3 cha wewe kutafuta pa kujishika, kutafuta kazi au connection. NB: Ni poa zaidi ukiwa na connection kabla ili mambo yakikaza una pa kujitetea au uwe na kanauli kakurudi ulipotokea.
Sasa baada ya kukaa kwa miaka mi3 either legally or illegally unakua qualified na hiyo “Arraigo Social” , hii imekaa hivi huwa wanaitoa kwa mtu yeyote aliekaa Spain kea miaka mi3 na zaidi.
Arraigo Social ina masharti yafuatayo;
1: Uwe umekaa Spain kwa muda usiopungua miaka mi3 ILLEGALLY.
2: Uwe una mkataba wa kazi , sasa inabidi uwe umejitetea na kupata kazi kwa muda huo.
3: Utatakiwa ku prove muingiliano wako kijamii na waSpain wenyewe , hii ina maana uwe na ndugu, jamaa, rafiki, jirani, mke, mme, mpenzi, au yeyote ambaye anaweza kuku backup.
4: Au pia kuna njia ya kufanya mtihani wa lugha ya Spain kama kigezo kimojawapo nadhani ni kama TOEFL au IELTS.
Kwa maelezo zaidi naambatanisha link pamoja na picha kadhaa za maelezo in details.
NB: Lengo la uzi huu na ule wa kwanza ni kuhabarisha ninayoyajua juu ya kutaka kuhamia nchi hizo mbili, nahitaji maelezo zaidi pia kea anae jua zaidi. Usikosoe tu weka inputs zako pia watu tuangalie fursa kwa upande huu.
Nawasilisha
9 Tips on How to Immigrate to Spain and Get Your Residence Permit