NJIA PANDA YA MAAMUZI SAHIHI

NJIA PANDA YA MAAMUZI SAHIHI

Joined
Oct 9, 2014
Posts
70
Reaction score
48
Habarini wakuu, Nachukua wakati huu kuomba ushauri wa nini niamue maana nipo njia panda na nahisi kuhitaji mawazo ya watu wengine juu ya hili swala.

Picha inaanza nikiwa kidato cha sita (2012) baada ya kukutana na binti mmoja ambae nilikua na mahusiano nae lakin yeye hakua mwanafunzi. Baada ya kufanya nae mapenzi yule binti alinambia kua anaujauzito wangu kupitia simu. Mimi sikumkatalia japokua nilipanik kidogo kwa vile nilikua bado mwanafunzi tena wa secondary. Wazo lililokua linanijia ni kwenda kuhakikisha kama kweli ni mjamzito na anaujauzito wa muda gani maana alinambia yu mjazito baada ya wiki mbili tu, tangu tulipotoka kufanya nae mapenzi. Kitu ambacho sikuamini ni kwamba yule binti alianza kunikwepa na sikufanikiwa kuonana nae paka namaliza shule. Baada ya mawasiliano nae kupitia simu ndani ya mwezi mmoja yule binti alipotea hewani na nikawa simpati kabisa na niliendelea kumtafuta kupitia namba yake lakini sikufanikiwa na mahali alipokua anakaa nilipokwenda kuulizia nikaambiwa hawamfaham kwani alikuaga anaenda kwa rafiki ake naye alishahama apo. Hivi majuzi tareh 26/06 mwaka huu kupitia facebook nikaiona account yake na bahati nzuri hakuwa amebadiri jina. Baada ya kumwomba ufriend naye akawa amenikumbuka so tukanza kuchat. Kitu alichoniambia ni kua ile mimba niliyompa alijifungua na hivyo ana mtoto wangu, Kwakweli sielewi nichukue maamuzi gani either nikubali au nikatae. Mbaya Zaidi huyo binti kumbe aliwahi kumwambia jamaa mwingine kua ndio mwenye ujauzito huo na hivyo uyo jamaa ndiye aliyekua anamhudumia paka alipojifungua. Kwa maelezo yake kwangu anadai baada ya kujifungua kulitokea ugomvi kati yake na huyo jamaa kwani ilionekana amejifungua kabla ya muda wakati mtoto ailizaliwa akiwa amekamilika (miezi tisa), hivyo ikabidi amwambie ukweli kua ile mimba haikua yake. Ila wakati huo huo uyo jamaa aliendelea kumtunza mtoto paka hivi majuzi baada ya kunipata mimi ndio akawa anagomea misaada ya huyo jamaa kwa mtoto akidai sio mtoto wake anaetunza. Hali ya kutokuelewana ilizidi kuwa mbaya baada ya vikao vya kifamilia kati yake na huyo jamaa adi wakafikia hatua ya kupelekana ustawi wa jamii. Maamuzi yaliyotoka ustawi ni kua binti yule anatakiwa yeye ndo agharamikie gharama za kwenda kufanya vipimo vya DNA kuthibitisha kua huyo mtoto sio wa huyo jamaa, na kiukweli yeye mwenyewe uyo binti amekiri kua hana uwezo wa kugharamikia ivo vipimo yeye kama yeye. Sasa bado natafakari nifanye nn juu ya hili swala maana hata ndugu zangu sijawaambia kutokana na utata uliopo kuanzia mimba na mgogoro wa mtoto mwenyew maana nyaraka zote kuanzia clinic na cheti cha kuzaliwa vimeandikwa jina la uyo jamaa ila uyo binti kila siku ananisisitizia kua yule mtoto ni wangu. Naombeni mawazo yenu wakuu maana sioni kupata maamuzi sahihi juu ya huu msala.

Naomba kuwasilisha.
 
Uckurupuke kuwa makin kwa hili ucfanyie mzaha kama VP Fanya umuone huyo mtoto kwanza kama INA wezekana mpeleke kwa mama ako au aunt yako anaweza tambua kimtindo kama kweli ni mwanao au laaah
 
Chunguza kwanza
mwanao ukimuona tu waweza jua bila kuhitaji DNA

na kama uko ready kumchukua ndo ufuate procedure
 
Hii story yajirudia nitatafuta Uzi huo niulete hapa..yaweza kuwa coincidence lakini mmmh sijui ngoja titaona.
 
Uckurupuke kuwa makin kwa hili ucfanyie mzaha kama VP Fanya umuone huyo mtoto kwanza kama INA wezekana mpeleke kwa mama ako au aunt yako anaweza tambua kimtindo kama kweli ni mwanao au laaah
Nliwaza kufanya Ivo ila paka saiv huyo binti haruhusiwi kusafir na uyo Mtoto paka itakapojulikana ni wa nani! Utata unakuja pale ntakapowambia ndgu zangu habar za Mtoto afu ikatokea kua si wangu.!!
 
C ukapime DNA Nan anaweza mwangalia mtoto kwa macho akajua wake, kama je mtoto kafanana na mama yake itakuweje, jitoe muhanga ukampime ujue kimoja afu pia mtoto wakuvutana mnamwaribu kisaikologia kama kashakua na akili
 
Funga safari mpaka waliko ukifika hakuna kuongea na mtu we mshike tako yule jamaa mnae scramble for and partition of child asiposhituka tu ujue mtoto wako mchukue.
 
Naona dalili za kufanywa kitega uchumi... Kama upo tayari kumchukua ukamlea mwenyewe Pima DNA na kwanini baba wa kambo amganganie ilhali hataki kutoa matunzo na sio wake??
 
Ni hapo utakapofanya vipimo vya DNA halafu ukute sio wako wala sio wa jamaa.
Hali ni ngumu eti kila mmoja anatafuta pa kuponea, sa ingine ukute wanaishi kwa amani na mumewe hayo mengine anayokuambia ni ya kusadikika tuu
 
Huyo anataka kukutumia kama daraja tu, ulipie kipimo cha DNA ila baba halisi wa mtoto yupo lakini hana pesa za kumudu kipimo cha DNA.
Ni vigumu kwa mwanamke alie na mimba yako kupotea kimyakimya na asikutafute mpaka uibukie facebook ndio akwambie hiyo mada.
 
Huyo anataka kukutumia kama daraja tu, ulipie kipimo cha DNA ila baba halisi wa mtoto yupo lakini hana pesa za kumudu kipimo cha DNA.
Ni vigumu kwa mwanamke alie na mimba yako kupotea kimyakimya na asikutafute mpaka uibukie facebook ndio akwambie hiyo mada.
kweli ndugu upo sahihi sana kwenye hili hapo atulie na alifikirie hili swala kwa kina sana.
kkk
 
Back
Top Bottom