Njia mpya ya utapeli yaibuka wakishirikisha Jeshi la Polisi bila kujitambua kuwa wanafanikisha dili za hawa matapeli

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
*JIHADHARI NA WIZI HUU MPYA*

Njia mpya ya utapeli yaibuka wakishirikisha Jeshi la Polisi bila
kujitambua kuwa wanafanikisha dili za hawa matapeli.

*mfano* : Matapeli wanaweza kukuuzia sim ya wizi ya bei kubwa ya kiasi cha shilingi laki nane ( 800,000/=) kwa fedha ndogo ya elfu sabini( 70,000/=) ili kukuingiza kingi ukiingia tu imekula kwako

Kwani simu hiyo unayouziwa ni ya mmoja wao (matapeli) na wanakuwa wamekopi Imei number ya simu hiyo sehemu.

Baada ya wiki wanakupigia ili kuangalia kama uko hewani. Huku wameshatoa ripoti polisi kuwa begi limeibiwa kwenye gari pamoja na vitu vingine na hiyo simu ikiwa ni mojawapo kati ya vitu vilivyoibiwa.

Na watatoa maelezo polisi thamani ya vitu vilivyoibiwa niTshs zaidi ya Milioni 7 (katika maelezo yake atakuwa ametaja laptop, fedha taslim na simu tatu au nne.)

Wanapewa mpelelezi na hapo ndipo Jeshi letu linajikuta limeingizwa kingi bila ya kujijua.

Mpelelezi anaomba msaada cyber crime kuitafuta simu hiyo.

Ikipatikana biashara inaanza . Unawekwa chini ya ulinzi kulipa vitu vyote ambavyo hujawahi hata kuviona na kesi ya wizi unayo.

Uongozi wa group unalishauri jeshi la polisi kuwa makini sana na hizi kesi za cyber. Labda mtakuja gundua kuwa simu hizi zinazotumika kutapelia watu zimekwisha ripotiwa mara mbili au tatu ndani ya miezi mitatu.

Ndugu zangu wanachama wa group hili msikubali kuuziwa simu mkononi ambayo ni used, na kama utanunua simu hiyo ambayo ni used basi mlipe kwa cheque, kagueni Imei number na umpige picha huyo aliyekuuzia pindi unapomkabidhi kiasi hicho cha Malipo.

Ikiwa hataki achana nae ndiyo salama yako.

Matapeli ni wengi sasa na wanabuni mbinu siku hadi siku ili kuyasukuma maisha yao.

Tunaitajika kuwa makini

Ahsanteni sana.
 
mbona tulishazungumza sana. "usinunue simu mkononi kwa mtu usiemfahamu"
 
Ahsante.. nimepata wazo fulani hapa ila halihusiani na utapeli mkaja niita saiba kraimu..
 
Tatizo linaanzia kwenye kupenda kitonga
Kwanini ukanunue simu kwa mtu, tena usiyemfahamu wakati maduka ya simu yamejaa tele.
Na wapigwe tuuu (in PMPP voice), wanapenda sana banana ganda
 
*JIHADHARI NA WIZI HUU MPYA*

Njia mpya ya utapeli yaibuka wakishirikisha Jeshi la Polisi bila
kujitambua kuwa wanafanikisha dili za hawa matapeli.

*mfano* : Matapeli wanaweza kukuuzia sim ya wizi ya bei kubwa ya kiasi cha shilingi laki nane ( 800,000/=) kwa fedha ndogo ya elfu sabini( 70,000/=) ili kukuingiza kingi ukiingia tu imekula kwako

Kwani simu hiyo unayouziwa ni ya mmoja wao (matapeli) na wanakuwa wamekopi Imei number ya simu hiyo sehemu.

Baada ya wiki wanakupigia ili kuangalia kama uko hewani. Huku wameshatoa ripoti polisi kuwa begi limeibiwa kwenye gari pamoja na vitu vingine na hiyo simu ikiwa ni mojawapo kati ya vitu vilivyoibiwa.

Na watatoa maelezo polisi thamani ya vitu vilivyoibiwa niTshs zaidi ya Milioni 7 (katika maelezo yake atakuwa ametaja laptop, fedha taslim na simu tatu au nne.)

Wanapewa mpelelezi na hapo ndipo Jeshi letu linajikuta limeingizwa kingi bila ya kujijua.

Mpelelezi anaomba msaada cyber crime kuitafuta simu hiyo.

Ikipatikana biashara inaanza . Unawekwa chini ya ulinzi kulipa vitu vyote ambavyo hujawahi hata kuviona na kesi ya wizi unayo.

Uongozi wa group unalishauri jeshi la polisi kuwa makini sana na hizi kesi za cyber. Labda mtakuja gundua kuwa simu hizi zinazotumika kutapelia watu zimekwisha ripotiwa mara mbili au tatu ndani ya miezi mitatu.

Ndugu zangu wanachama wa group hili msikubali kuuziwa simu mkononi ambayo ni used, na kama utanunua simu hiyo ambayo ni used basi mlipe kwa cheque, kagueni Imei number na umpige picha huyo aliyekuuzia pindi unapomkabidhi kiasi hicho cha Malipo.

Ikiwa hataki achana nae ndiyo salama yako.

Matapeli ni wengi sasa na wanabuni mbinu siku hadi siku ili kuyasukuma maisha yao.

Tunaitajika kuwa makini

Ahsanteni sana.
Wewe umeujuaje huu mchezo?
 
mbona tulishazungumza sana. "usinunue simu mkononi kwa mtu usiemfahamu"
Mmeshazungumza nyie na nani?

Mkamwambia nani?

Uka confirm vipi kwamba kila mmoja amesikia na kuelewa?

Kwa hivyo kama mmeshazungumza sana what's your point?

Kwamba uzi ufutwe?

Hebu nifungue hapo mkuu
 
Back
Top Bottom