Njia mpya ya kusafirisha "sembe" nje ya nchi

Njia mpya ya kusafirisha "sembe" nje ya nchi

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,347
Wauza sembe wamegundua njia mpya ya kusafirisha sembe kupitia JNIA kwa kutumia kampuni zinazosafirisha vifurushi. Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tizeba ameimbia Kamati ya Bunge ya Miundombinu iliyotembelea JNIA kuwa wiki iliyopita mamlaka husika uwanjani hapo zimekamata jumla ya vifurishi nane vilivyokuwa na dawa za kulevya.

Amesema jumla ya watuhumiwa nane wameshakamtwa kuhusiana na vifurishi hivyo na kuongeza kuwa wamiliki wa vifurushi hivyo bado hawajapatikana.

Amesema moja ya vifurishi hivyo kinapelekwa nchini Nambia huku kikionyesha kuwa kulikuwa na kitabu cha biology. Lakini kilipochunguzwa kilikutwa kikiwa na kiasi kikubwa cha heroin iliyokuwa imewekwa ndani ya kusasa za kitabu hicho.

Waziri ameongeza kuwa wauza unga pia wamekuwa wakitumia sandals na pakti za majani ya chai kusafirisha dawa za kulevya. Ameongeza kuwa vifurishi vingi vyenye dawa za kulevya vilikuwa vinaelekea nchi za Afrika Magharibi.

Habari kwa mujibu wa gazeti la Shanghai Daily la China.
 
in kwa sababu ya upuuzi with tutaendelea kuteseka. hatuna akili ndio maana Leo tunamshbikia lowasa awe raised wanchi kisa anajifanya wamekosana name jk. haiwezekani kwa tuhuma zote name kushindwa kazi kwa nzowa aendelee kuwepo jnia! sisi in wapuuzi, a cha tuendelee kuingizwa vidole machoni. INA maana hats anayepelekewa hafahamiki?
 
Hizo ni njia mpya au ni njia zilizokuwa zatumika tangu awali lakini wao ndio sasa wamezing'amua!!!!
 
huku kwetu bado sana, hizo note njia .za zamani tu.....
 
Katika Africa nzima Tanzania kwa sasa ndio ghala kuu la kupokelea "Sembe" baada ya kutoka shambani ie Pakistan,Brazil,Peru etc ila hasa kutoka Pakistan,chunguza unga mwingi unaoingia unatoka.nchi ipi halafu unganisha na wafanya biashara wakubwa hapa wenye asili asili na huko,unganisha uhusiano wa wafanya biashara hao na vyama vya siasa halafu jiulize kwa nini??!! Na pia tetesi za wana wa mfalme kuwa ma-director wa kazi hii!!

Ni aibu na fedheha kwa Taifa lakini ndio hivyo!!
 
Mmh! Hilo nalo neno
 
Sina hakika kama heroin na madawa mengine ya kulevya yanatengenezwa hapa TZ, so wakati tunajiuliza mbinu mpya ya kuyasafirisha nje, tujiulize pia yanaingiaje nchini?

Heroin inatengenezwa huko mbali halafu hiyo Heroin inaletwa Tanzania kwa sababu inchi yetu ni supplier mzuri kwa kutumia inlet na outlet zake zilizo salama kushinda mahala popote duniani
 
Njia hii ni ya muda mrefu tu, hawajaanza juzi wala jana.
 
Jamani kwanza kabisa naomba jina hili LISITUMIKE kabisa SEMBE hii ni lugha ya kuficha au kupunguza makali ya neno; kwa hapa siyo mahala pake! Hizi pia ni njia za kuhalalisha Madawa ya kulevya! Naomba itamkwe ilivyo haya ni MADAWA YA KULEVYA siyo SEMBE! Haya maneno kama Takrima = Rushwa yanafanya watu wasione kama ni kitu hatari.
Basi nirudi kwenye mada!
Mimi naona zoezi la kukomesha madawa ya kulevya liundiwe kikundi kazi tena kutoka jeshi la wananchi JWTZ maana vyombo vingine naona kama vimeshindwa.
 
Nia hii ni ya muda mrefu sana, nafikiri zilipendwa imepigwa tena....!

Kuna ile ya kuweka kwenye container! Nia hii kwa macho ya kawaida huwezi uona unga! Inabidi upime kwa nje (mwanzo wa container hadi mwisho wake) halafu upime tena kwa ndani (kuanzia mwisho wa container hadi mwanzo (kwenye mlango)! Tofauti utakayoipata ndio chumba unga ulipo! Mara nyingi wanachukua 0.5 hadi 1.0ft x upana x kimo.....!
 
in kwa sababu ya upuuzi with tutaendelea kuteseka. hatuna akili ndio maana Leo tunamshbikia lowasa awe raised wanchi kisa anajifanya wamekosana name jk. haiwezekani kwa tuhuma zote name kushindwa kazi kwa nzowa aendelee kuwepo jnia! sisi in wapuuzi, a cha tuendelee kuingizwa vidole machoni. INA maana hats anayepelekewa hafahamiki?

unaongea nini mjomba... Mbona hueleweki? Hebu soma tena post yako uone kama unajisoma!!
 
Sina hakika kama heroin na madawa mengine ya kulevya yanatengenezwa hapa TZ, so wakati tunajiuliza mbinu mpya ya kuyasafirisha nje, tujiulize pia yanaingiaje nchini?
genekai
===>hayawezi kujitengeneza yenyewe,nani anayatengeza?
 
Last edited by a moderator:
Sina hakika kama heroin na madawa mengine ya kulevya yanatengenezwa hapa TZ, so wakati tunajiuliza mbinu mpya ya kuyasafirisha nje, tujiulize pia yanaingiaje nchini?

Usije hata siku moja ukajidanganya kwamba hawafahamu! Wanafahamu sana mkuu ila sema tatizo ndo lile lile la siku zote la ''uenzetu'' na kitu kidogo juu!! Kwani huoni tembo wetu wanavyopukutika huko maporini wakati wao wako bandarini wanakamata makontena machache yaliyojaa vipusa wakati mengine mengi yakiwa yamepita? Changanya tu na za kwako mkuu na naamini utauona ukweli huu!
 
Back
Top Bottom