Xoldier
JF-Expert Member
- Mar 27, 2017
- 424
- 153
Napenda kuweka baadhi ya mawazo kidogo katika namna ya uendeshaji wa mahusiano ya mapenzi, yote ni katika kudumisha uhusiano wa kimapenzi uzidi kudumu kwa muda mrefu.
1: Kubembeleza, hii inafahamika sana na wengi pia wanatumia, ni njia nzuri ingawa ikitumiwa peke yake yaweza kuzoeleka na kuchokwa kwa haraka zaidi na mpenzi wako. Hii ni ile hali ya kunyenyekea mahusiano yenu kama mtu aliye umia sehemu ya chini ya mguu (nyayo) wakati wa kutembea.
2: Kibabe, Hii ni ile hali ya kulazimisha baadhi ya matukio kuendana na vile unavyo taraji. Haki sawa ipo ila isisahaulike kwamba sisi ni wa afrika na ni binadamu pia hivyo mfumo dume upo kwa namna yoyote ile, unapoamua kutumia demokrasia/kubembeleza pekee kwenye mahusiano ni vigumu kudumu kwa muda mrefu.
3: Kutembea juu ya akili, hii ni ile hali ya kuelewa nini kina maanishwa na mpenzi wako mwanzo wa mazungumzo na kutambua pia matarajio yake kutoka na swali au maelezo anayokupatia. Njia ni bora zaidi ukilinganisha na zote hapo juu maana ni msaada pia wa kulinda udhaifu(Defensive mechanism) wako, mfano mpenzi wako anaweza akakuuliza:
Msichana/Mwanamke: Unanipenda ???.
Swali hilo ni dogo sana ila lina maana kubwa sana na linaweza kuua au kukuza mahusiano, isiwe ni mazoea kujibu vile ambavyo anataraji unatakiwa kumfanya abadili namna ya kufikiri kidogo, hivyo waweza mjibu:
Mvulana/Mwanaume: Hapana
Kisha unatazama mapokeo yake kutoka na jibu ambalo hajatarajia, kisha waweza kuendelea kwa kusema
Mvulana/Mwanaume: Ni kweli sikupendi ila naishi ili nikupende.
Kama waweza zitumia njia hizo vyema nadhani hata kama huna hela itasaidia kulinda udhaifu wako pia ila utamtesa mwenzio kuteseka pamoja nawe.