NJIA 10 ZA MAFANIKIO KATIKA UJASIRIAMALI

fundichupi

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
382
230
Habari za jioni wana JF, nimeona nishee nanyi mawazo haya ambayo wengi wetu hatuyapi mkazo na badae tunakwama na kuhaha.
Kama wataka kufanikiwa katika uwekezaji wako na biashara hebu pitia haya machache ila yenye maana kubwa:-

1. uwezo wa kusimamia fedha.

kama huwezi kusimamia fedha, huwezi kusimamia biashara. Je, unajua ambapo fedha yako inakwenda kila mwezi? Je, unaishi chini ya kipato chako? Kama jibu la maswali haya ni hapana, itabidi ufanyie kazi namna ya kusimamia bajeti ya biashara.

2. Uwezo wa kuongeza fedha.

Kama unaweza kusimamia fedha, unaweza kupata zaidi? Ili kupata uwekezaji, unahitaji si tu kuelewa mahali pa kupata fedha, lakini jinsi ya kufanyia pesa hiyo biashara na kuongezea ikitokea shortage.

3: uwezo wa kukabiliana na matatizo.

Kama uwezo wako wa kutatua matatizo binafsi na vikwazo ni mdogo basi hutomudu hekaheka za biashara na utajikuta unakata tama kila mara. jifunze kuishi bila stress ama namna ya kufanya stress isiharibu utendaji wako

4. uwezo wa kuzalisha.

Hii ni nguzo kubwa, kwa sababu hakuna njia moja tuu ya namna ya kuwa mzalishaji bora. Inakubidi ukae chini ujitathimini unaweza nn hasa,unapenda nn hasa na utatumia vipi vilivo katika uwezo wako kujinufaisha na kujikuza ktk kipato na utendaji na ufanisi.

5. uwezo wa kupata marafiki.

Wanasema ndege wa jamii moja huruka pamoja, tafta na tengeneza rafiki ambao wapo katika tasnia yako ili upate kushauriana na kufundishwa zaidi. Binadamu anajifunza kwa kuiga siku zote, ukijiona bora na kwamba peke ako utaweza ni moja kati ya mia wanasimamaga. Ujuaji mwingi mbele kiza na ndio ninge inapokuwa majuto


6. uwezo wa kutambua uwezo na udhaifu.

Kama mmiliki wa biashara, huna haja ya kuwa mkamilifu katika kila kitu. Unachotakiwa kufanya ni kuelewa wapi wewe ni imara na wapi uko dhaifu. Kutathmini hili na kujijua kutakusaidia katika maamuzi ya biashara ya kufanya na namna ya kutatua changamoto zilizopo ktk sekta hio.


7. uwezo wa kuungana kupitia mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii huwakilisha sehemu muhimu ya mkakati wa masoko ya biashara yoyote kwa dunia hii mpya ya kiteknolojia. Si tu unahitaji kuelewa kila jukwaa/app,ila itakulazimu kujua mambo ya kimtandao ili kutumia fursa hii kujitangaza na kupata wateja wa mbali.

8. uwezo wa kuzingatia wateja wako.

Kuwa wazi, bila wateja, wewe huna biashara.Hakikisha ubora wa bidhaa na huduma ni kulenga mahitaji halisi ya wateja. Kama hujui nini ufanye tafiti na uliza maswali namna ya kuingiliana na wateja ili uwe na uwezo wa kutoa huduma kubwa kwa wateja.


9. UWEZO WA KUKABILIANA NA KUSHINDWA.

Hakuna mradi wa biashara ambao una mafanikio ya papo hapo; kujua jinsi ya kukabiliana na heka heka ni muhimu. Kumbuka kwamba kila mtu mwenye mafanikio huko nje alishindwa mara kadhaa kabla ya kupata ushindi. Kushindwa sio mwisho - ni darasa juu ya mafanikio.


10. Sehemu za kujitathimini

  • Communication Skills =High
  • Flexibility and Adaptability =High
  • Energy Level =Very High
  • Need for Achievement =Very High
  • Work Ethic = Very High
  • Honesty and Integrity =Very High
  • Initiative =Very High
  • Optimism =Very High
  • Self-Confidence =Very High
  • Tolerance of Ambiguity =Very High
  • Total Commitment =Very High

Kipengele hiki cha 10 si kuwatisha au kuwakatisha tamaa bali ni kwa ajili ya ww kujifanyia kazi haswaaa. Kuwa mwekezaji ni kazi kubwa, lakini yakupasa uwe fit katika yale 9 juu na ukubali kujifunza. Mafanikio yako ya baadaye yanategemea attitude yako.
 
Uko vizuri mkuu....

Tatizo ni wachache wanaoweza kufanya self-assessment kwa hicho kipengele cha 10
 
Back
Top Bottom