Njedengwa nyingine yatokea Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Njedengwa nyingine yatokea Dodoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kalikenye, Feb 11, 2012.

 1. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Wakati wakazi wa Dodoma wakiwa hawajasahau tukio baya la wananchi walalahoi, kubomolewa nyumba zao na kuachwa wakiwa hawana makazi, tukio jingine baya limetokea huko Dodoma la wananchi wa kima cha chini, kubomolewa nyumba zao na kuachwa wakihangaika bila ya makazi.

  Tukio hilo lililotokea siku ya Jumatatu ya tarehe 6/2/2012 usiku wa majira ya saa 10 alfajiri, limewakumba wakazi wapatao 11 wanaoishi katika shamba Namba 272 lililopo Mlimwa C, pembeni mwa mlima wenye makazi mapya ya Waziri Mkuu, huku vyombo vya habari pamoja na viongozi wa Kiserikali wakilipa Kisogo kana kwamba waliobomolewa ni wahalifu.

  Chanzo cha wananchi hao kubomolewa nyumba zao, ni mgogoro uliohusisha umiliki wa shamba namba 273 ambao ulipelekea kufunguliwa kwa kesi Namba 70/2011 katika Baraza la Ardhi na nyumba la Dodoma ambapo Baraza hilo liliamuru kuondolewa kwa watu wote waliovamia shamba hilo.

  Hata hivyo, jambo la kustaabisha ni kubomolewa kwa nyumba ambazo hazihusiki na mgogoro uliokuwa katika Baraza la nyumba.
  Lakini la kusikitisha zaidi ni jinsi Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wngine walivyowatekeleza wahanga hao bila ya msaada wowote kwa kisingizio cha kusubiri taarifa kutoka CDA ambayo haijapatikana kutokana na CDA kutokwenda eneo la tukio kwa ajili ya kupima.

  Aidha, habari zilizopo mtaani zinadai kuwa nyuma ya mgogoro huo, kuna Kigogo mmoja wa TRA Dodoma ambaye pia analinyemelea eneo hilo kwa ajili ya kulinunua na hivyo ndiye aliyegharamia zoezi zima la kubomoa nyumba za wananchi hao wasio na hatia.

  Jamani wana JF, shime nawaombeni tuungane kupinga uonevu huu uliopitiliza.

  Nawasilisha
   
 2. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Kwa wasiokumbuka, Ndejengwa ni eneo lililobomolewa nyumba katika eneo la Dodoma
   
 3. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Kitoto kichanga cha siku 2 ilibidi kiokolewe baada ya kuangukiwa na kifusi
   
 4. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Unyama huu unazidi kukua kila siku. Ila CDA wanapaswa kulaumiwa sana kwani ni kama vile hawayajui maeneo yanayostahili kujengwa na yale yanayopaswa kuwa wazi kwani watu hawa huwa hawajengi nyumba zao usiku. Hujenga mchana huku CDA wenyewe wakishuhudia lakini hukaa kimya.
   
 5. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Duuupz ARDHI ni "MARI YA SEREKARIIII"
   
 6. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kuna mshikaji wangu yuko Dom alinitonya juu ya kutokea kwa ubomoaji huo, lakini ajabu siaiona habari hiyo katika vyombo vya habari. Je, na wao wametiwa mfukoni?
   
 7. j

  jigoku JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Matunda ya utawala wa CCM!
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  this country !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! kizunguzungu
   
 9. T

  The Priest JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Msipende kuibua lawama zisizo na kichwa wala miguu,bila serikali kusimama kidete kila mtu atakuwa akijisikia anajenga mahali popote bila kufuata utaratibu,sisi wakazi wa Dodoma hatutaki ujenzi holela kwa sababu maendeleo hayaji kwa style hiyo..
  I dont support ujenzi holela kwanza unaingiza serikali kwenye matumizi ya pesa yasiyo ya lazima.
   
 10. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Mkuu kama umesoma vizuri habari hii, hoja sio ujenzi holela bali ni kutekeleza hukumu ya mahakama katika eneo ambalo halikuwa na mgogoro
   
 11. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Jamani any up dates jamani. Mwenye taarifa jamani juu ya hawa ndugu zetu. Wamefikia wapi kwenye issue hii.
   
Loading...