Nje ya 18 - Kagera Sugar VS Simba SC

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,188
8,215
Mungu aliumba dunia na maajabu yake, Mungu alimuumba Clatous Chama na kipaji chake, mpira umetupa tena sababu ya kutabasamu, baada ya Gaucho kuweka viatu kabatini, Diego Maradona kulala zake kaburini

Wachambuzi wapo katikati ya ubora wa Meddie Kagere, unafunguliwa ukurasa mwingine wa John Bocco, tunaenda kwenye tangazo tunarudi Chris Mugalu kaweka tena, ashike nani Top 10? Kila mtu anapeta

Hassan Dilunga was added in the group, Ndio kaingia tu leo na ameanza kutype, kaingia tu leo kaweka emoji za kufurahisha, Mwanaume sana wa kutambaa na chaki, winger sana wa kuificha mali, Thank you for the beautiful game Hassan

Thadeo Lwanga changed the group icon, ndio Thadeo leo kaubadili sana mpira, haikuwa rahisi katikati ya dimba bila yeye, leo kahakikisha mpira unatulia na ulinzi wa kati unadumishwa, kama sasa na siku zote na milele awapo Simba Sports

Mzamiru Yassin is typing....., Anataka kusema nini Selembe? Anaandika nini Kiungo punda? Anataka kusema kuhusu blocks zake? Interception zake? Au ubora wake siku ya leo? Anataka kusema kwanini hapambwi magazetini? Mwambieni yeye ndie Makelele wetu

Luis Miquissone is now the Admin, ndio kwanini isiwe hivyo, kwanini asiwe admn kama anatembea na sheria zote za Group, ukimkaba ni faulo, ukimuacha ni goli, kwenye nyasi za Kaitaba alifanya anachotaka, aliuita mpira nao ukaitika, akautuma nao ukatumika

Mohamed Hussein left the group, Mohamed Hussein was added.... Anataka kwenda wapi Captain? Atapatikana wapi Leftback kama yeye? Anaweza kupanda, anaweza kushuka, anaweza kukaa na mali na anajua kucheza na mawinga wagumu, what a man

Aishi Manula changed the group settings, anataka nini Aishi? Aishi anataka magolikipa wenye cleansheet tu wachat kwenye group, anataka Makipa wenye mikono salama sio tu Tanzania bali Afrika, another day, another Cleansheet Homeboy

Joash Onyango changed his profile photo, kaweka nini Joash? Kaweka picha ya Paolo Maldini kwenye DP, hataki kusema mengi bila shaka ukishaitazama majibu ushapata, hana maswali mengi

Manara kaweka status, inasemaje? "Wapo kileleni ila wanasikia joto".

jr_farhanjr_1619025521368.jpg
 
Mwenye rekodi ya assist na magoli ya mafisango naiomba....msimu wake wa mwisho ule
 
Back
Top Bottom