Mi ni mkristu lakini nilipewa stori moja ya mtume muhammad.Mtume alikuwa na tabia ya kwenda msikitini mara kwa mara.Jamaa mmoja kwa chuki zake binafsi akajenga katabia ka kujisaidia haja kubwa katikati ya ile njia apitayo mtume kwenda msikiti.Basi ikawa mtume kila akikiona kinyesi,alimshukuru mungu kwa kumshibisha yule aliyekunya,then atayazoa na kuyatupa kando.Basi siku moja mtume alishangaa kuona njia nzima iko safi,hakuna kinyesi.Mtume akaenda moja kwa moja nyumbani kwa yule mnyaji.Alipofika,alimjulia hali kisha akamuuliza,'vipi ndugu yangu unaumwa nini,maana sijaona yale mambo yako kwenye ile njia yangu ya kwenda msikitini?!'.