Njaa inakuja, Serikali CCM imejiandaaje???

nimetoka kanda ya kati Jana hakuna mvua kabisaaa.hapo yawezekana ikiwa njaa maana kanda ya kati.na juu kusini mikoa ruvuma rukwa.ndio ngao ya taiga kwa mahindi wasipo vuna vizuri tutanunu tsh2000.sembe
 
Si walisha ambiwa wakuu wa mikoa waizuie njaa? Sasa atakae tangaza njaa eneo lake, kukiona.
 
nimetoka kanda ya kati Jana hakuna mvua kabisaaa.hapo yawezekana ikiwa njaa maana kanda ya kati.na juu kusini mikoa ruvuma rukwa.ndio ngao ya taiga kwa mahindi wasipo vuna vizuri tutanunu tsh2000.sembe
Dar tayari Iko 1500
 
kwa dar kweli.sembe iko juu kuliko mchele
 
Wapo busy na ujenzi wa uwanja kwa mfalme ambao hauna faida yoyote lkn ukitumia mabilioni ..
Chama la mafisadi lililochoka kufikiri....
 
Sijui waziri wa kilimo nani maana naona kalala fofofo,bora wangemwaacha mwigulu angeshatoa way forward.

Inatakiwa waanze kuandaa kufungua akiba ya mahindi,
kwa mtu wa hali ya chini bei ya mahindi iko juu mno
Akisema kuna njaa anatumbuliwa kwani mmesahau ya Nimr
 
Njaa hailetwi na serikali ya CCM so msitegemee chochote kutoka kwetu mfanye kazi tu ya kulima kwa bidii kama mvua hakuna mje Dar es salaam na ndoo za kuchotea maji ili mchote maji ya bahari mkamwagilie hayo mazao.

Kama watu watajitolea tena kuwachangia walio na njaa hizo hela tutaenda kubireshea uwanja wa ndege wa CHATU.
no more comment.
 
Kweli hii ni No Comment
 
"nawateua lakini mkuu yeyote ambaye wilaya yake itakuwa na njaa atakiona" - anonymous
Mungu hadhiakiwi, unapomwambia mtu kuwa yeyote njaa ikitokea kwake atakiona utadhani mvua ni yake humtendei haki, na alisema yeye hana chakula cha msaada kwa mwenye njaa, huyu mtu tumfikirie mara mbilimbili huenda mungu anatuchapa kwa kukubali kutawaliwa nae.
 
Tatizo kubwa ni kutegemea kilimo cha mvua, ili takiwa kilimo kiwe cha umwagiliaji na cha kufwatiliwa na wataalam katika nchi, habari ya njaa tunge isahau
 
akili zilizojaa matope utazijua tu. pointi yako ni ya muhimu naweza sema katika mwaka Unaoanza January hakuna kitu kingine kitasulubu watanzania zaidi ya njaa. Shida yako umeleta thread hii kisiasa wakati huohuo ukitahadharisha isichukuliwe kisiasa. Nakuunga mkono kabisa hali ni mbaya sana hivi tunavyoongea na itazidi kuwa mbaya hata kama mvua zitanyesha vizuri baadae bado kuna muda wa zaidi ya miezi mitatu ya kusubiri kukomaa kwa mazao.
Niiombe serikali na hasa mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli akae na jopo lake la mawaziri na wataalam wa majanga watangaze hali hii kuwa ni ya hatari na hatua stahiki kukabiliana na hali hii zianze kuchukuliwa mapema.
 

Wakati unafanyika udhibiti wa kuuza mazao ya chakula nje ya nchi ulielewa nini???
 


Mentality za kimaskini sana hizi, tatizo la njaa unaona ni mkosi, na ukiugua utasema umerogwa. Akili za namna hii zinaweza kuja na suluhisho la tatizo??

Kinachomtofautisha mtu mweusi na rangi nyingine zote ulimwenguni ni pamoja na vitu kama hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…